6/recent/ticker-posts

Mabasi ya Umeme ni ya wananchi wanapaswa kuyatunza - Mbeto

 

MABASI ya Umeme ambayo yamewasili Zanzibar wiki iliyopita na yanatarajiwa kuanza kutoa huduma wakati wowote kuanzia sasa ni ya wananchi na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ni wakala anayefanyakazi na Serikali.
Akizungumza mara baada ya kurudi ziara ya kikazi nchini Spain katika Jiji la Madrid na Doha, Qatar alipokwenda kwa mwaliko maalum, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi na Uenezi Khamis Mbeto Khamis alisema mabasi hayo ni ya wananchi hivyo wana wajibu wa kuyatunza.
Alisema pesa iliyotumika kununua mabasi hayo ni kodi za wananchi ambao ndio wenye mabasi yao na ole wake atakayejaribu kufanya uharibifu wa aina yoyote katika mabasi hayo.
Alibainisha kuwa mabasi hayo ya kisasa yana kamera za usalama hivyo aliwaonya wale watakaothubutu kufanya uharibifu wowote kuwa watakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.
“Yatakuwa na ulinzi wa kamera ndani ya mabasi hayo na mtu ukipanda na wembe wako ukakata kochi, hatukuachi tunataka tubadilike, ukifanya uharibifu wowote katika lile gari utakamatwa” alisema.
Alisema mabasi hayo yatafika hadi nje ya Mji kutokana na zaidi ya kilometa 109 za barabara za lami zilizozingatia watumiaji wote wa barabara wakiwemo waenda kwa miguu, zilizojengwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
“Fly Over ya Amani na barabara zake ikikamilika itawezesha mabasi hayo kuunganisha Mnazi Mmoja, Chukwani hadi Bungu ambako barabara zake zimekamilika na zipo vizuri” alisema Mwenezi Mbeto.
Alisema Mwenezi huyo kuwa mabasi hayo mapya ni safari ya kuelekea Zanzibar mpya, tunayoitaka na kwamba maono ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni makubwa ambayo yanahitaji kupewa ushirikiano na awali kabla ya ziara hiyo alikuwa anashangaa kwanini nchini hatufanikiwi katika mambo mengi lakini alichogundua ni kuwa watu wanatakiwa kuwajibika na kufuata sheria zilizopo.

Alisema wenzetu wamejenga miji yao pamoja na mambo mengine, wanazingatia usafi na utunzaji wa miundombinu yao.
Mbeto aliwatoa wasiwasi watoa huduma za usafiri

Post a Comment

0 Comments