6/recent/ticker-posts

Mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa serikali juu ya kugharamia hatari za mabadiliko ya tabianchi na maafa




AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Ali Salim Matta, amewataka wadau na taasisi mbalimbali kuchukua jukumu la moja kwa moja katika kugharamia athari za mabadiliko ya tabianchi na maafa, akisisitiza kuwa suala hilo ni wajibu wa kila mmoja katika jamii.
Matta alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa serikali juu ya kugharamia hatari za mabadiliko ya tabianchi na maafa, yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Pemba.
Alisema madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha maafa makubwa na hata kuteteresha uchumi wa taifa katika juhudi za kurejesha hali ya kawaida baada ya majanga.
“Sote tuna wajibu wa kugharamia athari za mabadiliko ya tabianchi kabla, wakati na baada ya maafa. Hili si jukumu la Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais pekee kupitia Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, bali ni jukumu la kila mmoja wetu,” alisisitiza Matta.
Alifafanua kuwa bado kuna dhana potofu miongoni mwa baadhi ya wananchi kwamba masuala ya maafa ni dhamana ya ofisi hiyo pekee, jambo ambalo linahitaji elimu na uelewa mpana zaidi juu ya umuhimu wa kujiandaa kifedha kukabiliana na majanga.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame, alisema mafunzo hayo yametokana na tathmini maalum iliyofanywa na serikali, iliyobaini haja ya kuandaa mkakati mahsusi wa kugharamia mabadiliko ya tabianchi na maafa Zanzibar.
Alieleza kuwa matokeo ya tathmini hiyo yamepelekea kuandaliwa kwa mafunzo hayo kwa watendaji wa taasisi mbalimbali Unguja na Pemba ili kuwajengea uwezo wa kupanga na kutekeleza mikakati ya kifedha ya kukabiliana na majanga.
Makame alikumbusha kuwa mwaka 2017, Pemba ilikumbwa na mvua kubwa zilizosababisha uharibifu wa miundombinu, kuingia kwa maji ya bahari katika maeneo ya kilimo na kuharibu makaazi ya wananchi.
Akizungumzia athari za mabadiliko ya tabianchi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, mshiriki wa mafunzo hayo, Aisha Bakar Masoud, Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Pemba, alisema mwaka 2025 tani 20 za mwani ziliharibika katika eneo la Kiuyu Mbuyuni,


 

Post a Comment

0 Comments