Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi, wanafamilia na wananchi mbalimbali katika maziko ya Marehemu Theodosia Sylvester Mapunda yaliyofanyika leo, tarehe 23 Februari 2026.
Marehemu Theodosia Mapunda, ambaye ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo, amefariki dunia tarehe 21 Februari 2026.
Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyama vya siasa pamoja na wananchi.
Akitoa shukrani, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Cassian Gallos Nyimbo, amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa nia yake njema ya kuwaunganisha Wazanzibari na kuwa wamoja wakati wa faraja na misiba.





0 Comments