Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Mlezi wa Mkoa wa Tanga Kichama ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema Chama cha Mapinduzi kikiwa kinatimiza miaka 49 tangu kuzaliwa kwake kuna umuhimu mkubwa wa vijana kupatiwa Elimu juu ya historia ya CCM tokea kuasisiwa kwake hadi kilipofikia.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya Miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi yaliyofanyika katika Uwanja wa Stendi ya Bombani, Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Amesema Ikiwa Serikali inaendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo, vijana wanapaswa kujua msingi wa kuzaliwa kwa chama cha hicho jambo ambalo litawafanya kuishi kwa maono makubwa kama walivyokuwa waasisi wa chama ya Tanu na ASP.
Amefahamisha kuwa miradi mikubwa ya maendeleo ya kimkakati imejengwa Mkoani Tanga ambapo zaidi ya bilioni mia nne zimewekezwa kwa ujenzi wa Bandari ya Tanga, ujenzi wa barabara, hospitali na mpango wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Tanga unaendelea na umefikia katika ha
Mhe. Hemed ambae pia ni Mlezi wa Mkoa wa Tanga Kichama amewapongeza wanaCCM na wananchi wa Mkoa wa Tanga kwa kudumisha Amani wakati wote wa Uchaguzi na Baada ya uchaguzi mwa mwaka 2025 jambo lililochangia kupatikana kwa ushindi ya majimbo yote kumi na nne(14) yaloyomo Mkoani humo.
Amewaahidi wanachama wa CCM na Watanzania kwa Ujumla kuwa Chama cha Mapinduzi kitaendelea kusimamia na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa maslahi mapana ya Pande zote mbili za Muungano huo.
Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Komred Mfaume Kizigo amesema sifa za CCM ni nyingi zinazojuulikana kote Ulimwenguni ikiwemo kuhubiri umoja, Amani na Mshikamano ndani na nje ya chama hicho.
Komred Kizigo amefahamisha kuwa Busara na maelekezo mazuri ya Viongozi wa CCM akiwemo Mlezi wa Mkoa wa Tanga Kichama ndugu Hemed Suleiman Abdulla ndivyo vilivyopelekea CCM kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2025.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Mohammed Salim Ratco amesema Faida nyingi zimepatikana ndani ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM ikiwa ni pamoja na kukua na kuimarika kwa chama, kuimarika umoja na mshikamano kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi na wananchi wa Tanzania.
Ndugu Ratco amesema Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2025-2530 imetanua wigo mpana wa maendeleo katika sekta mbali mbali kama vile sekta ya Afya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, Bandari, Nishati ya umeme na maji safi na salama na miradi mengineyo inayoendelea kujengwa nchini kote.
Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe.. 05 / 02 / 2026.
0 Comments