6/recent/ticker-posts

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar haina ushahidi wa wizi wa baadhi ya mizigo

Mkurugenzi kuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na  Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao ya kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Terminal 3 Uwanja wa Ndege zanzibar.
Mkurugenzi kuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma  akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na  Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao ya kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Terminal 3 Uwanja wa Ndege Zanzibar.
-Mwandishi wa Habari wa Star TV Abdalla Pandu akiuliza maswali katika Mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma  kuzungumzia Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao kuhusiana na kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Taminal 3 Uwanja wa Ndege Zanzibar
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma  kuzungumzia Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao kuhusiana na kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Taminal 3 Uwanja wa Ndege zanzibar.
-Baadhi ya Vyombo vya Habari Vilivyohudhuria katika Mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Seif Abdalla Juma na  kuzungumzia Taarifa isio sahihi iliotoka katika Mitandao kuhusiana na kuharibiwa pamoja na  kuibiwa Baadhi ya Mizigo ya Abiria wanaoshuka Katika Uwanja Huo jambo ambalo sio la kweli na halina Ushahidi,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Terminal 3 Uwanja wa Ndege zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.11/02/2026.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imesema kuwa hakuna ushahidi uliyopatikana unaonesha uwepo wa wizi kwa baadhi ya mizogo katika viwanja hivyo

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Uwanja wa Ndege wa Amani Abeid Karume Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo  Seif Abdallah Juma amesema kuwa suala hilo halijabainika kutokana na Uchunguzi uliyofanywa

Aidha amesema kuwa kufuatia kadhia hiyo Mamlaka imechukua hatua za kuunda Kamati ya kufanya uchunguzi pamoja na kuwataka wachukuzi wa mizigo hiyo kuvaa kamera ili kubaini vitendo vyovyote vya wizi

Amesema kuwa Mamlaka imepokea malalamiko Desemba 29 mwezi uliyopita kwa baadhi ya wafanya biashara kuhusiana na kufunguliwa kwa baadhi ya mizigo yao jambo ambalo limetia wasi wasi na kupelekea kuundwa kwa Kamati hiyo

Aidha amefahamisha kuwa katika kufanya uchunguzi huo Kamati imebaini uwepo wa zaidi ya  mizigo 100 imekuja tayari imefunguliwa ambapo baadhi ya mizigo hiyo imeharibika 

Akizungumzia kuhusu kamera za kuchunguzia ameeleza kuwa katika Ndege eneo linalowekwa mizigo hakuna kamera hivyo ni vigumu kuona kinachofanyika huko

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha usalama wa mizigo Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa watu wa usalama wana haki ya kufungua mzigo na kuangalia kwa lengo la kuimarisha usalama wa abiria na mizigo

Kikao hicho kimefanyika kufuatia tuhuma za wizi zilizotolewa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari zilizokuja hivi karibuni

 

Post a Comment

0 Comments