Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiongoza mazoezi ya viungo ya Wiki ya Sheria katika Uwanja wa Mpira wa Gombani Chake Chake Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kuendelea kuwa karibu na Mahkama katika kupata haki zao na ellimu ya sheria jambo ambalo litawasaidia kuondokana na changamoto na vikwazo mbalimbali vinavyotokea kwa kutokujua sheria.
Ameyasema hayo katika matembezi ya wiki ya sheria yaliyoanzia Bank ya PBZ Chake Chake na kumalizia katika Uwanja wa Mpira Gombani Kisiwani Pemba.
Amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi walau dakika thelathini ( 30 ) kwa siku kwa lengo la kutunza afya na kuepuka magonjwa yasiyo yakuambukiza ikiwemo sindikizo la damu na kisukari ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kutokana na jamii kuacha tabia ya kufanya mazoezi.
Mhe. Hemed amesisitiza matumizi ya Tehama katika sekta ya sheria ili kurahisisha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi, kuondoa mianya ya rushwa na kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar amesema Mahkama ya Zanzibar imejipanga kuondokana na matumizi ya makaratasi na kuhamia katika matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha Mhe. Hemed ametoa rai kwa wadau wengine wa sheria kujielekeza katika matumizi ya TEHAMA ili kwenda sambamba na maboresho yanayofanywa na Mahkama, lakini pia kuendana na madiliko ya kimaendeleo ya teknolojia yanayokwenda kwa kasi duniani kote.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar amesisitiza wananchi kuendelea kutunza amani na mshikamano na kutambua kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba haki na wajibu inatendeka kwa wote kwa maslahi pamana ya Tana.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais na washiriki wote kwa ujimla kwa kushiriki katika matembezi hayo jambo linalodhihirisha umoja na mshikamano uliopo kati ya Watendaji wa Mahkama na Wananchi kwa ujumla.
Imetolewa leo na Kitengo cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe 08 / 02 / 2026
%20(1).jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
0 Comments