6/recent/ticker-posts

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aondoka nchini kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride la heshima wakati akiondoka Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Bole, Addis Ababa, nchini Ethiopia kurejea nchini Tanzania, leo tarehe 15 Februari, 2026.

Rais Dkt. Samia alikuwemo nchini humo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 14 na 15 Februari, 2026. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Miji na Miundombinu wa Ethiopia Mheshimiwa Chaltu Sani Ibrahim katika Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Bole, Addis Ababa, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 14 na 15 Februari, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi mbalimbali katika Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Bole, Addis Ababa, nchini Ethiopia kurejea nchini Tanzania, leo tarehe 15 Februari, 2026.


 

Post a Comment

0 Comments