6/recent/ticker-posts

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar awataka Wakandarasi Mradi wa Nyumba za Kisasa Chumbuni kushirikiana na Washauri Elekezi





 Wakandarasi na Washauri Elekezi wa Mradi wa Nyumba za Kisasa Chumbuni wametakiwa kufanyakazi kwa mashirikiano ili kurekebisha dosari zinazojitokeza katika Ujenzi wa Mradi huo.

Akizungumza katika ziara ya kikazi katika eneo la ujenzi kufuatia ripoti iliyoandaliwa na Washauri Elekezi wapya wa mradi huo kampuni ya Neo Design Consultancy Ltd, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar Ndg.Sultan Said Suleiman amesema hatua hiyo itawezesha kupiga hatua mbele na kuongeza ufanisi.
Aidha Mkurugenzi Sultan amesisitiza haja kwa pande zote mbili kuhakikisha ubora wa viwango na wakati wa kukamilisha Ujenzi huo.
Jumla Bloki 22 zenye Nyumba 1,095 zinajengwa katika awamu ya kwanza ya Mradi wa Chumbuni ambapo baadhi ya Majengo yapo katika hatua za kusakafiwa

Post a Comment

0 Comments