Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) wa mwaka 2026, Februari 13, 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia, chini ya Uenyekiti wa Rais wa Kenya, Mheshimiwa William Ruto.
Kikao hiki muhimu, kinachofanyika kuelekea Mkutano wa 39 wa Umoja wa Afrika (Februari 14-15), kinalenga kuharakisha hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha msimamo wa pamoja wa Afrika katika suala zima la mabadiliko ya tabia nchi.


0 Comments