6/recent/ticker-posts

Walimu wakuu wa skuli za maandalizi Msingi watakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.




Walimu wakuu wa skuli za maandalizi Msingi pamoja na washika fedha wa wilaya za Kusini na Kati, wametakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.
Hayo yameelezwa na mtendaji wa Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ( ZAECA) Sada Salum huko SKULI ya Kibele Sekondari wakati wa muendelezo wa Mafunzo yanayoratibiwa na Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi.
Sada amesema si vyema kwa walimu wakuu na wasimamizi wa fedha kufanya jambo lolote kitakalopelekea kujipatia kipato chochote ambacho kinatokana na Rushwa wanapokuwepo katika majukumu Yao.
Nae Mkurugenzi Idara ya Maandalizi na Msingi Fatma Mode Ramadhan akizungumza na watendaji hao amesema, ni vyema kwa walimu wakuu kuzitumia fedha vizuri, kusimamia Uwajibikaji wa walimu na kuondoa migogoro skulini.
Aidha amewataka washiriki kuyafanyiakazi Yale yote waliyofundishwa ili kuhakikisha wanazitekeleza vyema (KK3) yaani kusoma, kusoma na kuhesabu.
Mafunzo kama hayo tayari yameshafanyika katika wiliya zote za,Unguja.


 

Post a Comment

0 Comments