Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Ugonjwa wa Saratani unaendelea kuleta changamoto kubwa ya afya kwa umma Barani Afrika na duniani na kote .
Ameyasema hayo katika Mkutano wa kikanda wa kuwajengea uwezo nchi wanachama wa Wakala wa Kimataifa wa mionzi (IAEA) katika uchunguzi na matibabu ya Saratani kwa kutumia mionzi uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
Amesema kuongezeka kwa matukio ya saratani, pamoja na kikomo cha upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu katika maeneo mengi barani Afrika , kunahitaji kuimarishwa kwa uwezo, ushirikiano wa kikanda na matumizi bora ya sayansi na teknolojia.
Mhe. Hemed amefahamisha kuwa wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki una jukumu muhimu la kuhakikisha Mradi wa RAF6060 ambao unalenga kuimarisha uwezo kwa nchi Wanachama na kuboresha utambuzi wa matibabu ya saratani unafanikiwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, amesema kuwa mpango mkakati wa mradi huo nikusaidia katika upatikanaji wa rasilimali watu, kuimarisha uwezo wa watendaji sambamba na kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia katika dawa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza Mradi wa Kitaifa wa (URT 6033) wa kupanua na kuboresha matibabu ya saratani kwa kutumia mionzi pamoja na kuboresha huduma za Tiba ya Nyuklia na Tiba ya Mionzi ( Rediotherapy ).
Sambamba na Hayo Mhe. Hemed amewahimiza washiriki wote kushiriki kikamilifu kwa njia inayojenga ili mkutano huo utowe matokeo chanya katika kuimarisha mifumo ya Afya na huduma bora kwa watu wote Barani Afrika.
Kupitia ushirikiano na Wakala wa Kimataifa wa mionzi (IAEA) Mhe. Hemed amesema maendeleo makubwa yamepatikana ikiwemo upatikanaji wa dawa za nyuklia, Tiba ya Mionzi ( Rediotherapy ), fizikia ya matibabu na rediopharmacy jambo lililoleta ubora na ufanisi wa huduma za matibabu ya saratani.
Hivyo, amewasisistiza washiriki wa mafunzo hayo kuzidisha ushirikiano, kuwa wavumbuzi na wawajibikaji ili kuhakikisha kuwa faida za teknolojia ya nyuklia katika dawa ni salama, endelevu na zinapatikana kwa kwa watu wote wenye uhitaji.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu ambae pia ni Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. SAADA MKUYA SALUM amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Sekta binafsi inajipanga kujenga Hospitali ya matibabu ya saratani kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za matibabu ya saratani, dawa na vipimo kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa huo.
Dkt. Mkuya amesema Wizara ya afya imekusudia kuwapatia mafunzo watumishi wake juu ya namna bora ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa saratani pamoja na kuongeza rasilimali watu, vifaa tiba na madawa ili kupunguza changamoto ya kuongezeka kwa maradhi ya saratani.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mionzi Tanzani Dkt. EMMANUEL NGAILE amesema Ugonjwa wa Saratani unazidi kuwa janga kubwa Barani Afrika na kuendelea kupoteza maisha ya watu kutokana na kuwepo kwa changamoto ya tiba na upatikanaji wa dawa kwa wagonjwa wa saratani.
Dkt. Ngaile amesema mradi wa (RAF 6060) unajipanga kuhakikisha unasambaza taaluma ya matumizi salama ya mionzi, kutoa elimu juu ya ugonjwa wa saratani na kuziba pengo lililopo katika upatikanaji wa dawa na matibabu ya saratani kwa Tanzania Barana Zanzibar.
Imetolewa na Kitengp cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe..02 / 02 / 2026
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

0 Comments