6/recent/ticker-posts

Wizara ya elimu kundelea kutekeleza mkakati wa kusoma, kuhesabu, na kuandika



Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ndugu Khamis Abdulla Said amesema Wizara ya elimu inaendelea kutekeleza mkakati wa kusoma, kuhesabu, na kuandika ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na msingi mzuri tangu darasa la maandalizi.

Ameeleza hayo leo tarehe 2 February 2026 katika kikao kazi cha wadau wa tathmini ya kati ya (patnership compact) cheye lengo la kuangalia maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa mageuzi ya kipaumbele yaliyoainishwa kwenye mpango huo, kuelezea changamoto zilizojitokeza pamoja na kutoa muongozo kwa mipango ijayo ikiwemo kuibua miradi mipya, huko Madinatn al Bahar - Mkoa wa Mjini Magharib, Unguja.

Katibu Khamis amefahamisha kuwa ni vyema kila mwalimu kuanzia ngazi ya maandalizi, msingi na sekondari kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri na kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.

Amesema Zanzibar kwa sasa imefikia katika kiwango kizuri cha Elimu, ambapo matarajio ya kiwango cha ufaulu yamefikiwa kwa asilimia 92, hivyo wizara itaendelea kuimarisha sekta ya elimu kuanzia ngazi ya maandalizi ili kuhakikisha wanatekeleza vyema maagizo ya viongozi wakuu wa serikali pamoja na ilani ya Chama cha Mapinduzi.

kwa upande wao wawasilishaji katika kikao hicho wameelezea hatua mbali mbali zilizochukuliwa katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, ikiwemo kuwajengea uwezo walimu kwa kuwapatia mafunzo, kuzipatia skuli chakula kwa ajili ya wanafunzi wa maandalizi na msingi, kuwepo usawa katika upatikanaji wa vifaa skuli zote nchi na kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kulingana na mahitaji aliyokuwa nayo.

Nao washiriki wa mkutano huo wameipongeza serikali ya mapinduzi zanzibar kwa juhudi inazozicukuwa katika kuimarisha sekta ya elimu ikiwemo miundombinu, vifavaa pamoja na kuwapatia mafunzo walimu ili kuendana na wakati katika kutekelezaa majukumu yao.

Waraka wa makubaliano ya wadau katika kuleta mageuzi kwenye elimu ya msingi (partnership compact) baina ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na wadau wa maendeleo ambapo matayarisho yake yalianza kufanyika kuanzia september 2023,lengo ni kuondoa changamoto zilizopo na kuhakikisha wanafunzi wa maandalizi wanajua kusoma, kuandika, kuhesabu na kuwa wabunifu.  

imetolewa na:
kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano,
WEMA.


 

Post a Comment

0 Comments