6/recent/ticker-posts

Serikali itaendelea kusimamia Sekta ya miundombinu kwa kuimarisha usalama katika sekta ya Usafiri wa anga na bahari

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe Badria Atai Masoud amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itaendelea kusimamia Sekta ya  miundombinu kwa kuimarisha usalama katika sekta ya Usafiri wa anga,bahari na usalama wa vyombo vya moto ili kuwaletea maendeleo wananchi
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Amani Abeid Karume Uwanja wa Ndege nje kidogo mwa mji wa Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na Maendeleo ya Wizara hiyo
 Amesema kwa mwezi wa Januari sekta zote tatu zimeonyesha kuleta maendeleo chanya ya ukuaji kwa kuimarika kwa usimamizi na usalama sambamba na matumizi ya kiutendaji 
Akizungumzia sekta ya baharini Mhe Badria amesema kwa mwaka 2026 January jumla ya abiria laki mbili na elfu kumi nane mianane na kumi na tatu  wamehudumiwa kupitia safari mianne na mbili za meli ukilinganisha na mwaka 2025 kwa mwezi kama huo jumla ya abiria laki mbili elfu tano na kumi na tisa hivyo kumekuwa na ongezeko la asimllimia 6.7 kwa mwaka huu 
Amefahamisha kuwa kwa upande wa uingizwaji wa makontena kumeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia asimllimia 22 hivyo ongezeko hilo linaashiria kuimarika kwa biashara kitaifa na kimataifa 
Akizungumzia upande wa Shirika la Bandari Naibu amesema vyombo ambavyo vimesajiliwa ni miamoja na ishirini na tisa kwa mwezi wa Desemba 2025 ambapo kwa mwezi wa Januari 2026 kumeongezeka asilimia 18 pamoja na kupata ukaguzi wa meli za abiria na mizigo hali inayoonyesha kusimamia huduma hiyo kwa ubora
Ameongeza kuwa kwa upande wa sekta ya anga  mpango wa Serikali ni kuweka daraja kati ya terminal 2 na terminal 3 sambamba na kujenga terminal 4 na kukikarabati vyema kiwanja cha ndege cha kigunda kwa kufanya mbadala wa kiwanja cha Amani Abeid Karume 
Akizungumzia barabara Naibu Waziri amebainisha kuwa kuimarika kwa barabara kutasaidia kuunganisha masoko, kuengezeka kwa biashara, na kuongezeka kwa shughuli za utalii na kuvutia kwa wawekezaji kwani huleta maendeleo Mjini na vijijini
Hata hivyo amewataka madereva wa vyombo vya moto na wananchi kufuata Sheria za barabarani ili kupunguza ajali za barabarani sambamba na kuzitaka  mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kwa boda boda wenye kuchukua watoto wenye chini


 

Post a Comment

0 Comments