Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar imesema itaendelea kusimamia vyema Sera na juhudi za Serikali katika kudumisha Uhifadhi wa Bahari pamoja na viumbe hai vilivyomo ili kuvisaidia visitowkee na viweze kuishi kwa maisha endelevu ya baadae
Akizungumza katika hafla ya zoezi la uachiliaji wa Kasa Baharini lililofanyika huko Nungwi mnarani Aquarium mkoa wa kaskazini unguja Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Bi Mboja Ramadhan Mshenga amesema lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha viumbe hai wa Baharini wanalindwa kikamilifu ili wasitoweke lakini pia kuakikisha wanatumika kwa kuingiza kipato kwa wananchi kupitia utalii ili kukuza kipato chao na kuongeza pato la taifa
Aidha amewapongeza wavuvi kwa kuonesha kujali na kuthamini umuhimu wa kuhifadhi viumbe hai wa baharini kwa kuchukua juhudi za dhati za kuwafikisha kasa mikononi mwa serekali mara baada ya kuwavua kwa bahati mbaya wanapokua katika harakati zao za uvuvi huko baharaini
Pia ameipongeza Taasisi ya Nungwi Mnarani Aquarium kwa kuona umuhimu wa kuwatunza na kuwalinda kasa kwa kushirikiana na serekali kwa kupitia idara ya uhifahi wa bahari pamoja na kuwataka kulifanya zoezi hilo kuwa ni zoezi endelevu kwa maslahi ya taifa kwa ujumla.



0 Comments