THBUB yafika kijiji cha Dunga kuwapa elimu ya haki
za binadamu.
NA MWASHAMBA JUMA, (THBUB)
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, THBUB
ofisi ya Zanzibar, imewajengea uelewa mpana wanakijiji wa Dunga Kiembeni kuhusu
masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora.
Akizungumza
na wanakijiji hao kwenye mkutano wa pamoja baina ya Tume na wananchi wa Shehia
ya Dunga Kiembeni iliopo Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Afisa Sheria wa
THBUB Bw. Wilfred Msagati aliwahimiza wananchi hao kutambua haki zao na
kuzipambania pale zinapovunjwa.
Sambamba
na kuwaelekeza kufika Tume kwa lengo la kuwasilisha malalamiko yao endapo
watakupamba na masuala ya uvunjwaji wa haki na ukiukwaji wa misingi ya utawala
bora.
Wilfred
aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya “Majukumu ya THBUB” kwa wanajijiji
hao pamoja ya kuwaelimisha haki mbalimbali ambazo binaadamu zinamstahikia na
kumuwajibikia huku akiwafahamisha jinsi ya Tanzania ilivyoridhia mikataba ya
kimataifa kutekeleza haki za binadamu zikiwemo haki za watoto, haki za watu
wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.
Aidha, aliwaeleza wanakijiji hao,
mbali na majukumu mengi yanayotekelezwa na THBIUB pia Tume hiyo ina jukumu la kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za
binadamu, wajibu kwa jamii na kueneza nchini elimu kwa umma kuhusu haki za
binadamu na utawala bora.
Katika
mkutano huo pia, Wilfred aliwaeleza wanakijiji hao jukumu la THBUB kutembelea
maeneo mbalimbali ambayo watu huzuiliwa kwa lengo la kutoa elimu ya haki za
binadamu na misingi ya utawala bora, vikiwemo vyuo vya mafunzo na magereza,
maeneo yanayohifadhiwa wazee kwa lengo la kutunzwa na vituo vya kulelea watoto
yatima.
Naye,
Afisa Uchunguzi wa THBUB ofisi ya Zanzibar, Bw. Abdullatif Ali Sheha wakati
akiwasilisha mada ya “Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora” kwa wananchi
wa kijiji hicho, amesema lengo la mkutano huo ni kuwajengea uelewa wnanchi hao
ili watambue masuala ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya
utawala bora.
Pia
Bw. Abdul aliwahimiza wananchi hao kufika Tume kwa lengo la kuwasilisha
malalamiko yao pamoja na kuwaelewesha jinsi ya kuwasilisha mamalamiko hayo Tume
ili yapatiwe ufumbuzi.
Kwa
upande wa wanchi hao, waliishukuru THBUB na kuipongeza kwa jitihada zao za
kuwafikia wananchi wa vijijini pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Jumla
ya malalamiko manne ya wanakijiji cha Dunga Kiembeni yalipokelewa katika
mkutano huo yakiwemo matatu ya uvunjifu wa haki za binadamu na lalamiko moja
lilihusu ukiukwaji wa misingi ya utawala bora. Aidha, wananchi wengine
waliahidi kufika Tume kuwasilisha malalamiko yao.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
0 Comments