6/recent/ticker-posts

Ukaguzi Maktaba za skuli mpya zilizofunguliwa Pemba





 Wafanyakazi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar kwa upande wa Maktaba zake zilizo kuwepo pemba, leo wamefanya ukaguzi katika Maktaba za skuli mpya zilizofunguliwa Pemba. Ukaguzi huu ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za Maktaba na kukuza usomaji miongoni mwa wanafunzi.

Maafisa wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar kutoka Maktaba ilipo Chachani Chake Chake, walieleza umuhimu wa Maktaba katika kukuza Elimu na maendeleo ya jamii. Walitaja kuwa Maktaba zina jukumu muhimu katika kutoa huduma za usomaji na utafiti kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.
Ukaguzi huu unatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati ya Bodi ya Huduma za Maktaba na skuli hizo zilizofunguliwa , na kukuza huduma za Maktaba kwa wanafunzi.
Imetolewa katika Kitengo Cha Uhusiano - Bodi Ya Huduma Za Maktaba Zanzibar
BOHUMAZA

Post a Comment

0 Comments