Mkurugenzi Idara ya Tiba Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kambi ya Huduma za Afya na Vodacom Tanzania Foundation. kutoa huduma bure za upimaji wa afya kwa Wananchi, ushauri na elimu juu ya magonjwa yasiyo ambukiza kama shinikizo la damu na kisukari, (kulia kwake) Mkaimu Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.Julieth Magandi na (kushoto kwake) Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald .
Kambi hii ya huduma za Afya inatarajiwa kuendelea katika Mikoa mingine hivi karibuni.
Hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya New Amaan Complex Zanzibar, kwa mara ya kwanza kufanyika Zanzibar na itakuwa endelevu, iliyoaza 3-2-2026 na kumaliza kutoka huduma hiyo Ijumaa 6-2-2026 kwa Wananchi wa Unguja. 
Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kambi ya Huduma za Afya na Vodacom Tanzania Foundation. kutoa huduma bure za upimaji wa afya, ushauri na elimu juu ya magonjwa yasiyo ambukiza, kama shinikizo la damu na kisukari. kambi hiyo ya siku tatu iliyoaza 3-2-2026 na itamalizika 6-2-2926, inayofanyika katika viwanja vya New Amaan Complex Zanzibar.



0 Comments