Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amewataka wahitimu wa Mafunzo ya kujenga Taifa kuendeleza uzalendo pamoja na kuunga mkono juhudi mbali mbali zinazotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya vijana wa kujenga Taifa Katika Chuo cha Uongozi Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Dunga na kuwataka wahitimu hao kwenda kuyatumikia vyema Mafunzo waliopatiwa kwa muda wote waliodumu chuoni hapo na kuridhishwa kwa kufaulu vyema Mafunzo walipoatiwa.
Aidha Mhe.kitwana amesema itapotokezea fursa za ajira Serikalini vijana waliomaliza Mafunzo ya ujenzi wa Taifa watazingatiwa katika kupatiwa ajira pamoja na kuwaasa wahitim hao kuendelea kuwa Raia wema kwenye jamii ikiwemo kulinda amani na kujiepusha na madawa ya kulevya.
Mkuu wa Mafunzo luteni kanali Jaffari Khamis Juma kutoka Jeshi la kujenga Uchumi ( JKU) amesema Mafunzo hayo yalianza Tarehe 5 /03/2024 katika kambi mbali mbali za Unguja na Pemba na jumla ya Wanafunzi elfu moja mia tano na sitini na nane na kujifunza mafunzo ya Gwaride utimamu wa mwili masomo ya dasarani na kujifunza kivitendo katika kambi mbali mbali na uzalishaji mali.
Akisoma risala kwa niamba ya wanafunzi hao Rukia fadhili wahidi kuwa waaminifu na waadilifu pamoja kuyatumia vyema mafunzo waliopatiwa kwa muda wote waliodumu chuoni hapo na kujifunza masomo ya ujasiriamali kama vile mafunzo ya stadi za maisha ,kilimo, ufugaji ,ufundi wa uchomaji wa vyuma ,ufundi muashi na kushiriki katika shuhuli mbali mbali za kitaifa.





0 Comments