Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Abdi Talib Abdalla, akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu Mkuu wa Tatu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Prof. Idris Ahmada Rai pamoja na Wanataaluma kutoka Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni SUZA kwenye maadhimisho ya Miaka Kumi (10) ya Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Maadhimisho hayo yamefanyika Leo tarehe 14/02/2026 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla

0 Comments