Mkurugenzi Idara ya Sekondari Bi Asya Iddi Issa, amewasisitiza walimu kufanya ukaguzi wa ndani ya skuli ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Aliyasema hayo leo, tarehe 5 Febuari, 2026 wakati akizungumza na walimu wakuu wa skuli za sekondari wa mkoa wa kusini, katika ukumbi wa skuli ya kibele, mkoa wa kusini unguja.
Amesema walimu wanatakiwa waandae timu ya kufuatilia utendaji wa walimu wakiwa shuleni kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu.
Bi Asya amewataka walimu wafanye tathmini ya ufaulu wa kidato cha nne 4 na kuandaa mipango kazi kwa kufata mtaala mpya ili waweze kuongeza nguvu kwa masomo yaliokuwa hayajafanywa vizuri.
Nae Mkuu wa divisheni ya sekondari, Mwalimu Mfaume Jafar Mfaume, amewapongeza walimu kwa kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha 4 kwa asilimia kubwa na kuwataka waongeze juhudi zaidi kwa wanafunzi wanaokuja ili kuongeza ufanisi.
Aidha amewasisitiza kuhamasisha wanafunzi kuitunza miundombinu ya skuli pamoja kuweka mikakati na sheria madhubuti kwa ajili ya utunzaji wake, ili itumike kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari Mawasiliano na Uhusiano (WEMA).


0 Comments