Afisa Mdhamini wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Mfamau Lali Mfamau amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kila Kijana wa Zanzibar anakuwa na Shuguli ya kufanya itakahayomuingizia kipato na kutokuwa tegemezi kwa familia
Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa maafisa wa Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar kwa ngazi ya Shehia zote za Pemba amesema ili kufikia hatua hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameanzisha Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji ambapo Vijana watakua fursa ya kusema na Aidha kutatuliwa changamoto zao kwa haraka na usahihi.
Aidha ametoa wito kwa Vijana kuitumia fursa ya kuanzishwa kwa Wizara hiyo kuzungumza changamoto zao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na uwezeshaji katika biashara na kupatiwa mafunzo na mitaji itakayowasaidia Vijana kujiongezea kipato Chao cha kila siku.
Akizungumzia mafunzo hayo amewataka maafisa hao kusimamia Uchaguzi huo kwa uweledi na ufanisi mkubwa huku wakizingatia Uchaguzi huo unafanyika kwa huru, haki na maslahi ya Vijana
Aidha ametoa wito kwa Vijana kuchagua Viongozi wenye uthubutu na uwezo wa kuwasemea changamoto zao na wenye Uzalendo wa kuipenda Nchi yao.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan amesema Uchaguzi wa mabaraza ya vijana kwa Ngazi ya Shehia ni muhimu ili kupata viongozi ambao watakuwa msaada mkubwa wa kuleta maendeleo katika Shehia zao na Taifa kwa Ujumla
Aidha amesema mafunzo hayo wanayopewa maafisa wa Uchaguzi wa mabaraza kwa ngazi hiyo yatawasaidia maafisa hao kusimamia Uchaguzi huo kwa kufuata utaratibu na kanuni za Uchaguzi za Baraza la Vijana Zanzibar
Pia amezitaka Kamati zilizoteuliwa Kusimamia Uchaguzi huo kutambua nafasi zao na jukumu walilopewa la kuufanya Uchaguzi huo unafanyika bila ya kuwepo ubabaifu na kuhakikisha Vijana wanatumia fursa hiyo kwa kuchagua na kuchaguliwa bila ya kujali tofauti zao za Kisiasa, Kijamii na Kiutamaduni walizonazo
Wakati huo huo Mratib wa Baraza la Vijana upande wa Pemba Hafidh Khamis Rajab amewataka Vijana wenye nia ya kugombea nafasi za Uongozi



0 Comments