6/recent/ticker-posts

Waziri wa Fedha aongoza Kikao kati ya Serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa njia ya mtandao



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameongoza Kikao kati ya Serikali na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa njia ya mtandao, akiwa jijini Dodoma, kuhusu mapitio ya Tathmini ya utekelezaji wa Program ya Extended Credit Facility-(ECF), yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.1, inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya Programu ya Serikali ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Dirisha la Resilient and Sustainable Fund (RSF) yenye thamani ya dola za Marekani milioni 786.2
Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, Bw. Nicolas Blancher,, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. Mbayani Saruni, na wataalamu wengine wa Wizara ya Fedha na IMF.


 

Post a Comment

0 Comments