Afisa Mikopo wa Chuo cha Zanzibar School of Health (ZSH), Ndg. Mahmoud Maktuba Haji, akipokea tuzo ya Utendaji bora
Afisa Mikopo wa Chuo cha Zanzibar School of Health (ZSH), Ndg. Mahmoud Maktuba Haji, akisikiliza kwa makini akiwa kikao cha Maafisa Mikopo wa Vyuo vya Tanzania kilichoandaliwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB),
Picha ya pamoja ya washiriki
Afisa Mikopo wa Chuo cha Zanzibar School of Health (ZSH), Ndg. Mahmoud Maktuba Haji ameshiriki kikao cha Maafisa Mikopo wa Vyuo vya Tanzania kilichoandaliwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB), kinachofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 10 hadi 13 Februari katika Ukumbi wa ZSSF, Chake Chake, Pemba.
Katika kikao hicho, Ndg. Mahmoud Maktuba Haji amepokea tuzo ya Utendaji Bora kwa niaba ya Chuo cha Zanzibar School of Health, ikiwa ni kutambua mchango na ufanisi wa chuo katika utekelezaji wa masuala ya mikopo ya elimu ya juu.
Kikao hicho kinalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Maafisa Mikopo, kujadili na kupendekeza maboresho ya mifumo ya mikopo, pamoja na kuwajengea washiriki uelewa mpana kuhusu masuala ya mikopo kwa maendeleo ya sekta ya elimu.



0 Comments