Na Mwandishi Wetu, SUZA
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewatunuku vyeti wahitimu 145 wa mafunzo ya wahudumu wa afya ya ngazi ya jamii (CHW) yaliyowajengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa jamii.
Mafunzo hayo ya miezi sita yamewashirikisha wanawake 131 na wanaume 14 ambao wamejifunza kutoa huduma kwa uweledi zaidi kama vile kupima sukari, maradhi ya moyo, huduma za lishe za watoto na kukusanya takwimu.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Makamu Mkuu wa SUZA, Prof. Abdi Talib Abdalla, Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba-SUZA Dk. Ali Adnan Idarous, aliwahimiza wahitimu hao kufuata miongozo waliyojifunza ya utoaji huduma bora bila ubaguzi wa aina yoyote.
Katika mahafali yaliyofanyika viwanja vya Skuli ya Afya iliyoko Mbweni tarehe 7/02/2026, Prof. Abdallah aliwakumbusha wahitimu hao wanapokwenda kufanya kazi kwenye jamii watalazimika kufuata miongozo kama walivyoelekezwa kwenye mafunzo waliyoyapata, kuibua changamoto na kuzifanyia kazi sambambana na kuwasaidia wananchi kwa moyo wao wote.
Vile vile, walijifunza namna ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza na pia kutunza siri za wagonjwa. Mafunzo hayo ni endelevu na yanaendelea kwa wanafunzi wengine wapya 100.



0 Comments