Ameyasema hayo, wakati wa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi wenye uhitaji katika Hospitali ya Wilaya Kitogani, ambao umetolewa na Kikosi cha zimamoto na Uokozi Zanzibar (KZU).
Aidha amesema pia ni kuwaunga mkono Wanawake kwa vitendo kutokana na kutambua juhudi za mama katika kulea familia na kuchangia maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mrakibu Muandamizi kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar (KZU) Bi Asha Othman Said amesema lengo la kutowa msaada huo ni kusaidia Wazazi na Wajawazito.
Aidha amawataka wanawake kuchukuwa tahadhari ya juu ya matumizi ya moto hususan katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo kuunguwa moto.
Akizugumza kwa niaba ya daktari wa zamu, kitengo cha akinamama Hospitali ya Wilaya ya Kitogani Suleiman Khalid khamis amesema msaada huo, umeleta hamasa kwa Wazazi na wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
Huku baadhi ya wanufaika, wametoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwawekea mazingira bora ya huduma za Afya ikiwemo, Hospitali za kisasa na Vifaa tiba kwa ajili ya kujifunguwa.
Dawati la Jinsia katika Kikosi cha Zimamoto na Uokozi, limekabidhi vitu mbalimbali ikiwemo, Sabuni na Pempas kwa wajawazito, Wazazi sambamba na kufanya Usafi.








0 Comments