Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia Waumini wa Dini ya kiislam katika Masjid Ouweys Fuoni Kibondeni Wilaya ya Magharibi " B " Unguja mara baada ya Ibada ya Swala ya Ijumaa.
Ameyasema hayo wakati akiwasalimia waumini wa masjid Ouweys Fuoni Kibondeni Wilaya ya Magharibi “ B “ mara baada ya kumaliza Ibada ya swala ya Ijumaaa.
Amesema suala la kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu kunapelekea kuwaweka wananchi pamoja na kuishi kwa umoja , upendo na mshikamano baina yao.
Alhajj Hemed amefahamisha kuwa maendeleo serikali imekuwa ikitekeleza ujenzinwa miradi mbali mbali ya maeneleeo ikiwemo miundombinu ya barabara, masoko ya kisasa, skuli za ghorofa na mahospitali kwa lengo la kuimarisha ustawi wa maisha ya wananchi wa Zanzibar.
Amewataka wananchi wa Zanzibar wakiwemo wakaazi wa fuoni Kibondeni na maeneo jirani kutoa ushirikiano kwa serikali pamoja na wakandarasi wanaojenga miradi ya maendeleo ili kuweza kufikia malengo ya serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wote.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewasisitiza waumini wa dini ya kiislam na wazanzibar kwa ujumla kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo nchi ili kuweza kuviwezehmsha vizazi vijavyo kufaidi matunda ya serikali yenye amani na tulivu ndani yake.
Akitoa khutba ya swala ya Ijumaa Sheikh Adam Ali Haji amewataka waislamu kuyaendeleza yale yote waliyoyafanya katika mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo kufanya ibada kwa wingi na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa nyakati zote.
Sheikh ADAM amewasisistiza waumini wa dini ya kiislam kujitahidi kuwa pamoja na watu wenye mahiaji maalum ikiwemo mayatima kwa nyakati zote ili kuweza kupata fadhila kutoka kwa ALLAH ( S.W )
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Leo tarehe..27 / 03 / 2026.
0 Comments