6/recent/ticker-posts

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Suleiman Abdulla Amewataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei za Bidhaa

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia Waumini wa Dini ya kiislam katika Masjid Sogea uliopo Sogea Branch Wilaya ya Mjini Unguja mara baada ya Ibada ya Swala ya Ijumaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewataka wafanya biashara kutopandisha bei bidhaa za vyakula ili kila mwananchi aweze kujikimu hasa katika kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani.

Ametoa wito huo wakati akiwasalimia waumini wa Masjid SOGEA uliopo SOGEA BRANCH Wilaya ya Mjini  Unguja  mara baada ya kumaliza Ibada ya swala ya Ijumaaa.

Amesema mwezi wa ramadhani ni mwezi wa kuchuma thawabu kwa kutendeana mema na kusaidiana hivyo ni vyema kwa wafanya biashara kufuata bei elekezi ambazo zitamuwezesha kila mwananchi kujipatia iftari pasipo na usumbufu wowote.

Makaumu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Zanzibar amewataka wananchi kuendeleza utamaduni wa kusaidiana lakini pia kwa wenye uwezo kutoka kwa ajili ya makundi maalumu na wasiojiweza ili nao waweze kutimiza ibada ya funga kwa utulivu..

Amesema kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeweka punguzo kwa kila bidhaa ili kuweza kuwasaidia wananchi kupata huduma mbali mbali kwa wakati na kwa bei nafuu hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani na matayarisho ya skukuu ya Idd el Fitri.

Sambamba na hayo Alhajj  Hemed amewataka waumini kukithiririsha kuisoma Qur-an na kufanya ibada kwa wingi hasa kwa masiku haya yaliyobakia ili kuweza kupata fadhila za mwezi mtukufu wa ramadhani pamoja na kujiweka karibu na Allah ( S.W )

Alhajj Hemed amewataka Wananchi kuendelea kudumisha Amani na Utulivu uliopo Nchini pamoja na akuiombea dua nchi iepukane na majanga mbali mbali ikiwemo vita, ukame, maradhi na mengineyo.

Akitoa khutuba ya swala ya Ijumaa Ustadh Khamis Gharib Khamis amesema kuwa amekula hasara Yule ambae unamalizika mwezi wa ramadhani akawa ameshindwa kujikurubisha kwa Allah kwa kufanya matendo mema ambayo yatamuwezesha kulifikia lengo la kufunga.

Ustadhi Khamis amewasisistiza waumini wa dini ya kiislam kumuelekea Allah ( S.W ) katika shida zote kwa kufanya ibada kwa wingi ikiwemo visimamo vya usiku hasa katika masiku yaliyobakia katika mwezi huu mtukufu wa ramadhan.

Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe ..06 / 03 / 2026

Post a Comment

0 Comments