6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR--IFTAR NA WANANCHI WA KIKWAJUNI--SHEIKH IDRIS ABDULL WAKILI KIKWAJUNI

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendeelea kuwathamini na kuwapa kipaombele wananchi wote wakiwemo wananchi wa kikwajuni waliopisha ujenzi wa nyumba za maendeleo.

Hayo yamesema na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Alhajj.Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya Iftar  iliyoanadaliwa na shirika la nyumba Zanzibar ( ZHC ) Kwa wananachi wa kikwajuni iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdull Wakili Kikwajuni Zanzibar.

Amesema kuwa mashirikianao waliyoyatoa wananchi wa kikwajuni kwa serikali ni ya kupigiwa mfano hivyo serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inayoongoza na Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi itahakikisha wananchi hao wanapewa kipaombele na wanarejea katika nyumba hizo mara tu ujenzi huo utakapo kamilika.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amaesema nyumba hizo zitajengwa katika viwango vya hali ya juu na kuwawezesha wananchi kupata makaazi bora na salama ambapo amewataka wananchi hao kuwapuuza wale wote wanaopotosha juu ya ujenzi huo na marejeo yao katika nyumba hizo.

Mhe. Hemed amesema kuwa dhamira ya serikali ya awamu ya nane (8) ni kuwawekea mazingira wezeshi wananchi wote wa Zanzibar na kuifanya nchi iwe na muonekano wa kisasa jambo litakalozidi kuipaisha Zanzibar kitaifa na kimataifa.

Sambamaba na hayo ameendelea kuwashukuru wananchi wa   kikwajuni kwa uamuzi wao wa kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa na kuwaahidi kuwa serikali itaheshimu  makubaliano waliyokubaliana kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Nae katibu mtendaji kutoka ofisi ya mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume amewashukuru wananchi wa kikwajuni kwa kuwa tayari na kushirikiana na serikali kwa kupisha ujenzi wa mradi mkubwa wa nyumba za maendeleo ambazo zitawawezesha waannchi hao kuishi katika mazingira safi na salama.

Sheikh Khalid amesema hatua kubwa za kimaendeleo zinazofanywa na serikali kwa wananchi wote wa Zanzibar inaonesha wazi kuwa serikali ina nia thabiti ya kubadilisha maisha ya wazanzibari hivyo wananchi wanapaswa  kuiombea serikali ili iweze kufanya makubwa zaidi kwa maslahi mapana ya vizazi vya sasa na baadae.

Imetolewa na kitengo cha habari ( OMPR )

Leo tarehe….07 / 03 / 2026.

Post a Comment

0 Comments