Maombi hayo yalifunguliwa na baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama Cha ACT- Wazalendo Majimbo ya Uchaguzi waliyoshindwa kisiwani Unguja wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwa mwaka katika majimbo hayo.
Hukumu hiyo imetolewa na Mhe. Jaji Moh’d Ali Moh’d, ambapo mahakama imeamua kufuta mashauri hayo baada ya kuyapitia na kuyafanyia tathmini kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi,
Mahakama Kuu ya Zanzibar ilikubaliana na pingamizi zilizowekwa na upande wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kwamba maombi hayo yalikuwa na kasoro nyingi za kisheria.
Mahakama ilijiridhisha kuwa hati za kiapo (affidavits) zilizoambatanishwa na maombi hayo zilikuwa na kasoro za kisheria, na hivyo haziwezi kutambuliwa wala kuwa sehemu ya maombi yaliyowasilishwa mahakamani.
Kutokana na kasoro hizo, Mahakama iliamua kuyatupilia mbali maombi hayo.

0 Comments