6/recent/ticker-posts

Waziri Haroun azungumza na waandishi siku 100 za Mafanikio ya Uongozi wa Dkt. Mwinyi





 Na Maelezo Zanzibar  05.03.2026

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano Tanzania imefanikiwa kutekeleza kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa kuwafikisha huduma hiyo karibu na wananchi wa Unguja na Pemba

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusiana na siku 100 za Mafanikio ya Uongozi wa Dkt. Mwinyi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman amesema jumla ya wananchi 680,184 wamepata huduma hiyo, wa kiwemo wanaume 312,954 na wanawake 367,230.

Amesema katika kampeni hiyo jumla ya migogoro 749 imepokelewa wakiwemo ya ardhi, mirathi, ndoa, ajira, udhalilishaji na ukatili wa kijinsia pamoja na matunzo ya watoto ambapo migogoro 259 imetatuliwa papo kwa hapo

Kwa upande wa Mahakama Waziri Haroun ameeleza kuwa Serikali imeimarisha muhimili wa mahakama kwa kuongeza idadi ya majaji, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa haki na kusogeza huduma za mahakama karibu zaidi na wananchi.

“Juhudi kubwa zimefanywa za kuimarisha muhimili wa mahakama kwa kuongeza idadi ya majaji kutoka majaji 8 mwaka 2021 hadi kufikia majaji 14 mwaka 2025, wakiwemo wanawake 5 na wanaume 9, miundombinu ya mahakama inaendelea kuimarishwa kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa kajengo ya Mahakama za mikoa na wilaya kwa Unguja na Pemba ili kuimarisha upatikanaj wa haki na kusogeza utoaji wa huduma karibu na wananchi.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uendeshaji wa kesi, jumla ya kesi 7,352 zimesikilizwa, huku idadi ya kesi ikipungua kwa asilimia 30.7 katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023.

Akizungumzia Afisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Dkt. Haroub ameeleza kuwa Ofisi hiyo kupitia Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) imefanikiwa kuokoa na kudhibiti jumla ya sh. Bilioni 27.82 na dola za kimarekani 35,341 kati ya fedha hizo bilioni 26.37 na dola za kimarekani 30,542 zilirudishwa Serikalini na bilioni 1.45 na dola za kimarekani 4,799 zilirejeshwa kwa wananchi.

“Vile vile katika kipindi cha miaka mitano Ofisi kupiti ZAECA ilifanikiwa kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo 233 Unguja naPemba yenye wastani wa thamani y ash.trilion 2.29 na dola za Kimarekani milioni 85942 ili kuona utekelezaji wake kwa kuzingatia ubora wake na thamani halisi ya fedha katika miradi hiyo” amefahamaisha Waziri Haroun.

Kwa upande wa ZAECA, Wizara imeendelea kufanya kazi kwa karibu na miradi mikubwa ya serikali kwa kuweka utaratibu wa ufuatiliaji ili kupunguza vitendo vya rushwa na kuhakikisha fedha za serikali zinalindwa na kutumika ipasavyo.

Waziri amesema serikali ina mpango wa kufanya tathmini ya utendaji wa watumishi ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, ukizingatia maslahi ya wafanyakazi kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.

Aidha, amesema Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu baadhi ya watumishi na viongozi, na kusisitiza kuwa hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Waziri Haroun amewataka watumishim wa umma kufuata sheria na kanuni za utumishi na kudumisha uwajibikaji ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Post a Comment

0 Comments