6/recent/ticker-posts

Mwakilishi wa Jimbo la Jang'ombe, Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amewataka wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao kusoma Qur-ani

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Jang'ombe,  Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amewataka wazazi na walezi kuwahimiza  watoto wao kusoma Qur-ani ili kuibua  vipaji vya kuhifadhi Qur-ani jambo ambalo litasaidia kujenga  misingi imara ya  kumcha Mungu.

Ameyasema hayo wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur-ani yaliyoandaliwa na Al-Madrasatul Wakfiyatul Islamiya huko Kwa alinatu, Wilaya ya Mjini.
Amesema kuwa mashindano hayo ni njia muhimu ya kuwahamasisha watoto kujifunza na kuipenda Qur-ani, sambamba na kuwajengea msingi mzuri wa maisha yao ya baadaye.
Aidha amewapongeza walimu na waandaaji wa mashindano hayo kwa jambo zuri walilolifanya   kwa juhudi kubwa ya kuwahifadhisha Qur ani wanafunzi wa chuo hicho yatayosaidia  kukulia katika maadili mema  ya kiislamu 
Akisisitiza  Jamii kuendeleza kusoma qur ani Kwa wingi  Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani mwezi ambao umeshuka Qur-an ambayo ni uongofu kwa waumini 
Amefahamisha kwamba Katika  mambo matatu muhimu ya kuyatekeleza ni kutoa sadakatul jaria, kupata elimu yenye manufaa ambayo ukawafundisha na wengine pamoja na kuwa na mtoto mwema ambaye atakuombea dua .
Nao  Waandaaji wa mashindano hayo wamesema lengo la kuandaa mashindano hayo ni kuwahamasisha watoto kujifunza, kuhifadhi na kuzingatia mafundisho ya Qur-ani katika maisha yao ya kila siku ili iweze kuyafaa duniani na akhera .
Kwa Upande wa Sheha wa  Shehia ya Kwaalinatu Salmini Shaabani Mzee amesema amepata faraja kuona katika Shehia hiyo kuzalishwa vipaji vya kuhifadi Qur-ani  na kuwashukuru walioandaa jambo  hilo.
Mashindano hayo yamewakutanisha wanafunzi kutoka madrasa mbalimbali ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali pamoja na pesa taslim  kama ishara ya kutambua juhudi zao katika kuhifadhi Qur-an
mashindano ya kuhifadhi Qur-ani  yaliyoandaliwa na Al-Madrasatul Wakfiyatul Islamiya  yakifadhiliwa na Vikosi cha Valentia Zanzibar 'KVZ' pamoja na Tropical Air.


Imetolewa na Kitengo cha Habari .
WHSUM.

Post a Comment

0 Comments