6/recent/ticker-posts

Naungana na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuomboleza kifo cha Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani.

Mheshimiwa Lukuvi atakumbukwa daima kwani alikuwa Kiongozi mchapakazi na mzalendo, aliyetoa mchango mkubwa kwa Taifa Letu, Jimbo lake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)

Ninatoa salamu za pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, Waheshimiwa Wabunge, Familia ya Marehemu, Ndugu, Jamaa, Marafiki, na Wananchi wote wa Jimbo la Isimani.

Raha ya Milele, umpe ee Bwana, na Mwanga wa Milele umuangazie, apumzike kwa amani. Amina.

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Post a Comment

0 Comments