Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), akipokea tuzo maaalum kutoka kwa Mlezi wa Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association - TAWiFA) ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Ikulu Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, kama Ishara ya kutambua mchango wake kwa Chama hicho, wakati alipofika kufungua Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), ulioandaliwa na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association - TAWiFA), katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha, ambapo aliwapongeza wanawake katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na katika kuchangia maendeleo nchini katika sekta mbalimbali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), akionesha tuzo maaalum aliyopewa na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association - TAWiFA), kama Ishara ya kutambua mchango wake kwa chama hicho, wakati alipofika kufungua Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Ikulu Zanzibar ambaye pia ni mlezi wa chama hicho, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (kushoto) na Rais wa Chama hicho, Bi. Fikky Ntomola.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(Kulia), akimkabidhi Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bi. Sauda Msemo, tuzo ya shukran kwa kudhamini Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), ulioandaliwa na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association - TAWiFA), katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(Kulia), akimkabidhi Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, tuzo ya shukran kwa kudhamini Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), ulioandaliwa na Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association - TAWiFA), katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha.

Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati aliyeketi), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanawake katika Sekta ya Fedha Tanzania (Tanzania Women in Finance Association - TAWiFA), baada ya hafla ya kufungua Mkutano wa Tatu wa Wanawake katika Sekta ya Fedha (Women in Finance Conference 2026), ulioandaliwa na Chama hicho, katika Jengo la Papu Tower, jijini Arusha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Arusha)





0 Comments