Habari za Punde

UZINDUZI WA KAMPENI YA CHAMA CHA CUF VIWANJA VYA KIBANDAMAITI

MGOMBEA Urais wa Chama cha CUF Seif Sharif akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar wa Chama chake katika Viwanja vya Kibanda maiti.
`Mgombea Uwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akimnadi mgombea wa Urais Zanzibar kupitia CUF.

Meneja Kampeni wa CUF, Salum Bimani akitowa sera za chama chake katika mkutano wa kampeni viwanja kibanda maiti.


MgombeaUrais kupitia CUF Seif Sharif Hamad akionesha ilani ya Uchaguzi ya chama chake baada ya kukabidhiwa na Makamo Mwenyekiti wa CUF Machano Khamis Ali.
Waangalizi wa Kimataifa wa uchaguzi wakifuatilia mkutano wa CUF wa uzinduzi uliofanyika viwanja vya Kibanda Maiti.
Wanachama na wapenzi wa Cuf wakiwa katika viwanja vya Kibanda maiti katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni.
Wanawake wa CUF wakicheza ngoma ya Bomu katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni.

Wandishi wa Habari wakiwa makini kutafuta picha bora ya magazeti katika mkutano wa CUF wa uzinduzi wa kampeni ya Urais wa Zanzibar.

Kikundi cha Matarumbeta kikitowa burudani katika uzinduzi wa kampeni Viwanja vya Kibandamaiti.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwasili katika Viwanja vya Kibanda maiti
Kikundi cha Brass bend kikiongoza Maandamano ya uzinduzi wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar

WANACHAMA wa CUF wakiwa katika maandamano ya Uzinduzi wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar iliofanyika Viwanja vya Kibanda maiti.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.