Taasisi zaidi Muungano zijenge ofisi Zanzibar - Dk. Karume
Afungua jengo la ofisi ya Makamu wa Rais
Na Mwandishi wetu
KUNA umuhimu mkubwa kwa taasisi zaidi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kujenga majengo ya ofisi zake Zanzibar, ili kuimarisha utendaji wa taasisi hizo.
Wito huo umetolewa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, alipofungua jengo jipya la ofisi na makaazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Dk.Karume alisema umuhimu wa kujengwa ofisi hizo unakuja kutokana na kuongezeka haja na shughuli za ofisi hizo, katika kuimarisha utekelezaji wa kazi zake na mambo ya muungano.
Rais Karume aliipongeza ofisi ya Makamu wa Rais chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohammed Shein, kwa kujenga jengo hilo la kisasa Zanzibar, ambalo ni kielelezo cha mapenzi yao kwa Zanzibar.
Aidha Dk. Karume alimpongeza na kumshukuru aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Daudi Balali kwa uamuzi wake wa kujenga ofisi ya kisasa ya taasisi hiyo, huko Kinazini Mjini Zanzibar.
Mbali ya kusifia usanifu na ujenzi wa jengo hilo, Dk. Karume alihimiza utunzaji wa majengo hayo na kueleza umuhimu wa kutengwa bajeti maalum ya matunzo na uendelezaji wake.
Akizungumzia ujenzi wa ofisi na makaazi hayo, Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais, Ruth Mollel, amesema umegharimu zaidi ya shilingi za Tanzania, bilioni 10.3, ambapo zaidi ya bilioni 8.6 ni kwa ujenzi na zaidi ya bilioni 1.7 ni za utaalamu.
Mollel alieleza kuwa ujenzi huo ulioanza Julai 2007 na kumalizika mwaka huu, umefanywa chini ya ukandarasi wa kampuni ya Railway Jianchang Engineering ya China na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam.
Nae Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib, alisema ujenzi wa ofisi hiyo ni muendelezo wa hatua za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujenga ofisi zake za kudumu Zanzibar.
Alizitaja miongoni mwa ofisi hizo kuwa ni Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, ofisi ya uhamiaji na nyumba ya mapumziko Madungu kisiwani Pemba, ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kinazini na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano huko Tunguu.

No comments:
Post a Comment