Habari za Punde

CCM YAZOA VITI VINGI VYA UWAKILISHI MJINI.

CCM yazoa viti vingi Uwakilishi mjini



Na Mwantanga Ame

TARUMBETA za vuvuvela jana zilitumika kufanyia mbwembwe katika kituo cha Afisi ya Tume ya Uchaguzi ya Wilaya ya Mjini, baada ya Tume hiyo kutangaza matokeo ya uchaguzi katika majimbo tisa ya wilaya hiyo.

Aliyekuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alitoa kali ya aina yake kwa kuingia ndani ya ukumbi kituo cha Afisi hiyo kupokea matokeo ya kura zilizopigwa juzi kwenye zoezi la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Tume hiyo ilimtangaza Hamza kuwa mgombea mteule wa Uwakilishi jimbo la Kwamtipura na kufanikiwa kulitetea vyema, baada ya kujipatia ushindi mzito wa kura 5,139 na kumgarakaza mgombea wa Chama cha CUF, aliyepata kura 233.

Msimamizi wa kituo cha Wilaya Mwanapili Khamis, akitangaza matangazo hayo huko skuli ya Chekechea ya Miembeni, alisema alimtangaza Hamza hali iliyosababisha vuvuzela kurindima kwenye ukumbi huo kwa furaha kutoka kwa mashabiki wa CCM.

Wakati Matokeo hayo yakitangazwa hakukuwa na vyama vya upinzani ambavyo vilishuhudia matangazo hayo na kuufanya ukumbi huo kutawaliwa zaidi na wagombea wa Chama cha Mapinduzi kwa nafasi ya Uwakilishi waliokuwa wakisindikizwa na washindi wa Chama hicho kwa ngazi ya Ubunge.

Msimamizi huyo alisema Jimbo la Kwahani alieibuka a ushindi kw nafasi ya Uwakilishi Ali Salum Haji, aliepata kura 5,021 na kumshinda mgombea wa CUF aliyepata kura 1,259 ambapo katika jimbo la Jang'ombe Suleiman Othman Nyanga naye aliibuka kidedea kwa kujipatia kura 5,884.

Katika jimbo la Mji Mkongwe, mgombea wa CUF, Ismail Jussa Ladhu, alipata kura kura 4,566 na kumuangusha Simai Mohammed Said, aliyepata kura 1,667.

Katika jimbo la Kikwajuni Kikwajuni,mgombea wa CCM, Mahmoud Mohammed Mussa aliibuka kidedea kwa kupata kura 4,493, huku katika Jimbo la Chumbuni Mwakilishi wa zamani Machano Othmani Said naye akiipeperusha vyema bendera ya CCM kwa kupata kura 4,901 na kumuangusha mgombea wa CUF aliyepata kura 3,874.

Katika jimbo la Jimbo la Magomeni, Mwakilishi anayetetea nafasi yake kutoka CCM, Salmin Awadh Salmin, aliibuka na ushindi mzito wa kura 5,036 na kumfyeka mgombea wa CUF aliyepata kura 3,363.

Katika Jimbo la Rahaleo, msimamizi huyo alisema kuwa aliyeshinda ni Nassor Salum Ali (Al-jazira), baada ya kupata kura 3,952 na CUF kujipatia kura 2,310 na Mgombea wa Jimbo la Mpendae Mohammed Said Moahammed aliepata kura 4,858.

Fatma Mbarouk Said, CCM katika Jimbo la Amani ameibuka kuwa mshindi baada ya kupata kura 4,627 na Khamis Rashid Abeid, amepata kura 2,145

Katika nafasi za Udiwani, msimamizi huyo alisema wadi ya Mkunazini imechukuliwa na CUF, huku zilizobakia zote zikiwa zimechukuliwa na CCM.

Akichambua takwimu hizo alisema Wadi ya Chumbuni anamtangza rasmi mgombea Juma Ngwali Juma, ambaye alishinda kwa kupata kura 1692 na kumshinda mgombea wa CUF aliepata kura 1,292.

Wadi ya Mwembemakumbi, Msimamizi huyo alisema imeoongozwa na mgombea wa CCM, Mussa Haji Indrisa aliepata kura 3582 na kumshinda Mgombea wa CUF, aliepata kura 1,972, huku Wadi ya Kwaalinato imeongozwa na Fatma Suleiman wa CCM aliepata kura 3,322 na CUF wamepata kura 565.
kiendelea alisema kuwa Wadi ya Jang'ombe imeoongozwa na Mgombea wa CCM kupitia Mgombea wake Saleh Fasih aliepata kura 2,622 na kumshinda mgombea wa CUF kwa kura 1,486.

Wadi ya Kikwajuni alisema alieshinda mtetezi wa Wadi hiyo ambaye sasa ni Meya wa Mji wa Zanzibar Mahboub Issa Juma aliepata kura 2,212 huku mgombea wa CUF alipata kura 1,178 na Wadi ya Mikunguni imeenda kwa Awena M. Mkubwa wa CCM aliopata kura 2306, na CUF imepata kura 295.

Alieleza kuwa Wadi ya Magomeni alieshinda ni Harir Abdalla Bori wa CCM aliepata kura 1,216 na kumshinda mgombea wa CUF aliepata kura 606 na Wadi ya Mkunazini alieshinda ni Nassor Hamid Said, CUF aliepata kura 2,105 na Wadi ya rahaleo alieshinda niAmeir Makungu aliepata kura 1,819 baada ya kumshinda mgombea wa CUF aliepata kura 1082.

Wadi ya Mlandege alieshinda ni Mgombea wa CCM Khamis Mbarouk Khamis alieshinda kwa kura 2,261 na Mgombea wa CUF alipata kura 1,997.

Nae Msimamizi wa Wilaya ya Kusini Maalim Suleiman Haji Hassan, Jimbo la Makunduchi alieshinda ni Haroun Suleiman wa CCM aliepata kura 6,454 Mzee Ameir Mussa wa CUF aliepata kura 1,145.

Jimbo la Muyuni Msimamizi huyo alisema kuwa Mgombea wa CCM nafasi ya Uwakilishi kwa Jimbo hilo Jaku Jussa alipata kura 5,995 huku mpinzani wake kutoka chama cha CUF Suha Suleiman alipata kura 1,315.

Upande wa Wadi alisema, Wadi ya Mtegani alieshinda ni Maryam Sleiman Haji wa (CCM) aliepata kura 1231 na Wadi ya Mzuri alieshinda ni Zawadi Hamdu wa (CCM) na Mtende ni (CCM), Kizimkazi ni Mussa Bahorera wa (CCM)

Kibigija (CCM) na Pandu Haji Mjaka wa (CCM).

Maeneo mengine ambayo CCM iliweza kupata viti kuongoza katika kipindi cha miaka mitano ni ya Wadi ya Muungoni mgombea wake Jecha Shaaban Jecha alishinda kiti hicho na Paje ni Mzee Rajab Mzale huku

Sleiman Haji Vuai alishinda Wadi ya Muyuni na Mgombea wa wadi ya

Kikadini, Issa Mwinyi Shauri kutoka (CCM) aliibuka kuwa mshindi pamoja na Wadi ya Bwejuu, ilichukuliwa na chama hicho.

Uchaguzi wa Wadi ya Kajengwa, ni miongoni mwa ulioakhirishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, baada ya kujitokeza hitilafu katika karatasi za kupigia kura kutokana na baadhi yake kujichanganya kwa picha na majina halisi yaliotumika katika zozei hilo.

Kutokana na kujitokeza hilo, Tume hiyo imepanga kuendesha uchaguzi huo Novemba 28, 2010, ambapo utazishirikisha Wadi ziliomo katika Jimbo la Kikwajuni, Mji Mkongwe, Magomeni na Kwahani kwa upande wa Unguja na Pemba ni Wadi ya Chanjaani, Wara na Vitongoji.

Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, msimamizi wake Thabit Idarous Faina, alisema kuwa alieshinda ni Mbarouk Mussa wa CCM aliepata kura 3,552 na kumshinda mgombea wa CUF Vuai Kona Haji aliepata kura 1, 627.

Majimbo ambayo CCM inayaongoza katika Wilaya hiyo alisema ni pamoja na Tumbatu, Chaani, Matemwe na Jimbo la Nungwi limeenda CUF

Wilaya ya Kaskazini 'B' Majimbo ambayo CCM imeweza kupata majimbo ni ya Jimbo la Kitope, Bumbwini na Donge.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.