Habari za Punde

UJENZI WIZARA YA FEDHA PEMBA WAHOJIWA

Na Radhia Abdalla, Pemba

MWENYEKITI wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadhi, ameitaka Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Pemba, kuchukua hatua zinazofaa ili kulipatia ufumbuzi tatizo la ujenzi wa ofisi ya wizara hiyo ambao umesita kwa muda mrefu sasa.

Awadh aliyasema hayo wakati wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea ujenzi wa afisi ya Wizara hiyo Pemba ambao umesita baada ya jengo hilo kuporomoka na hivi sasa limewekewa mwega ili lisiendelee kuporomoka.

Aliitaka wizara kutoa maelezo ya kutosha juu ya hatua ambazo zimeshachukuliwa kwa mkandarasi na msimamizi wa ujenzi wa ofisi hiyo.

Alisema jengo hilo linaonekana dhahiri kuwa halitoweza kutumika kutokana na kufanya nyufa kubwa licha ya serikali kutoa fedha nyingi kujengwa jengine.

Naye Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Bakari Haji Bakar, alisema wizara yake itachukuwa hatua na taratibu zinazofaa kubaini chanzo cha ucheleweshwaji wa ujenzi wa ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.