Habari za Punde

MWAKILISHI, MBUNGE MAKUNDUCHI WAWAWEZESHA WANAFUNZI

Na Ali Mohamed, Maelezo

MWAKILISHI na Mbunge wa Jimbo la Makunduchi wamewawezesha wanafunzi wa skuli za jimbo hilo waliofaulu kuingia kidatu cha tatu na cha tano pamoja na michipua kwa kutoa fedha taslim shilingi 4,100,000.

Akikabidhi fedha hizo kwa wanafunzi hao, Mwakilishi wa Jimbo hilo amabaye pia ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman, alisema kwa niaba ya kiongozi mwenzake wamefarajika sana kutokana na kiwango hicho cha kufaulu.

Skuli ya sekondari ya Kajengwa ambayo ni miongoni mwa skuli nane zilizomo ndani ya jimbo hilo na Makunduchi ndio iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kidatu cha pili mwaka 2010/2011.

Aidha alitoa wito kwa wanafunzi hao kujali zaidi masomo ya sayansi hasa hesabati kwa vile ni somo ambalo linamuwezesha mwanafunzi kufaulu kwa kiwango cha juu (Division 1) ambapo bila kufaulu somo hilo kupata ufaulu wa kiwango hicho kwa mwanafunzi inakuwa ni ndoto.

Aliwataka wazazi kushirikiana vyema na walimu kuendeleza jitihata za kuimarisha elimu kwa wanafunzi ndani ya jimbo hilo huku akitoa ahadi kuwa yeye na viongozi wenzake watakuwa mstari wa mbele katika masula ya elimu kwa wanafunzi.

Nayo kamati ya Kuendeleza Elimu Jimbo la Makunduchi (JUKEJIMA), ilifahamisha kuwa jimbo la Makundichi lina historia kubwa kielimu kwa vile wataalamu na viongozi wa ngazi mbali mbali wametoka katika eneo hilo.

Aidha wajumbe wa kamati hiyo waliwashukuru na kuwapo Mwakilishi na Mbunge wa jimbo hilo kutokana na jitihada zao kubwa za kushrikiana na wananchi kutatatu changanmoto za elimu na kuleta mafanikio ambayo yanaonekana na wananchi wa ndani na nje ya jimbo hilo la Makunduchi.

Nae Mwakishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji Vuai Khamis Juma alisema skuli ya Kajengwa imefanya vizuri sio kwa kupasisha wanafunzi wengi tu bali imefanya vizuri kwa wastani wa masomo yote kwa vile mchakato wa kupata skuli bora unaangalia kufaulu katika viwango vya masomo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.