Awataka waepuke kukitia aibu chama, viongoziAshangaa wabunge, wawakilishi kutoelewana  
Na Mwantanga Ame
MAKAMU wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, amewaeleza wabunge wa CCM kukwepa janga la kuwatia aibu viongozi wa chama hicho kwa kuzomewa na kushushwa kwenye majukwaa kwa aibu.
Balozi Seif alisema aibu hiyo inaweza kutokea kwa viongozi wa CCM kushushwa kwenye majukwaa na kuzomewa endapo wabunge hao watashindwa kutekeleza ahadi walizoziweka kwa wananchi.
Makamu huyo alieleza hayo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Farahani mjini Dodoma, iliyowajumuisha wabunge wa CCM, ambayo ilikuwa na lengo la kubadilishana mawazo.
Alisema aibu hiyo inaweza kuepukwa endapo wabunge hao watatambua wajibu wao wanaotakiwa kuufanya kwa wananchi kwa kuhakikisha wanakuwa watumishi bora sambamba na kuzitimiza ahadi zao.
“Ndugu zanguni msipokuwa makini kwa kutoteleza majukumu yenu, mnaweza kumtia aibu Rais wa Zanzibar kwa kuzomewa ama kushushwa majukwaani pale atakapokuwa anawadi kama wagombea”, alisema.
Balozi aliwaeleza wabunge hao kuwa lazima wazingatie na kulifanyiakazi suala hilo kwani matokeo ya aina hiyo yalionekana katika maeneo mengi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, jambo ambalo lilimfanya mgombea wa Urais wa CCM Dk. Jakaya Kikwete, kujikuta kwenye wakati mgumu.
Alisema sababu kubwa ya kujitokeza mambo hayo ilitokana na baadhi ya viongozi waliochaguliwa na wananchi kutoonekana katika majimbo huku ahadi walizozitoa kushindwa kuzifanyia kazi.
Kuwepo kwa hali hiyo Balozi Seif, alisema Chama cha Mapinduzi hakitapenda kuona hali hiyo inajirejea tena katika uchaguzi mkuu wa 015, na ni lazima wabunge na wawakilishi wa CCM, kuhakikisha wanatimiza ahadi zao za kuwatumikia wananchi.  
Alisema Chama cha CCM kwa kuthamini wanachama wake wawe katika hali nzuri  hivi sasa tayari mfuko wa maendeleo ya Jimbo umeanza kuwapatia wabunge ambazo zitasaidia kuhudumia majimbo ambapo wabunge wote wa Zanzibar wataweza kufaidika nao.
Balozi Seif, alisema nia ya serikali ya Muungano kutoa fedha hizo ni kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanatimizwa katika miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya majimbo na sio kutumiwa vyenginevyo hasa kuangalia maslahi binafsi ya Mbunge.
Alisema hivi sasa mkakati ambao watalazimika kuufanyiakazi ni kuhakikisha wanamaliza tatizo la ukosefu wa vikalio katika maskuli yaliopo katika majimbo yao kwani hiyo ni moja ya ahadi ambayo ameitangaza rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein ambapo utekelezaji wake utakuwa unawahusu wabunge na wawakilishi.
Alisema inasikitisha kuona tatizo hilo baadhi ya viongozi wa majimbo bado hawajaweka deski hata moja katika skuli walizonazo kwenye majimbo yao jambo ambalo wanapaswa kuona aibu kwani haipendezi kuendelea kuwaacha wanafunzi kukaa chini maskulini.
Alisema ni jambo la kwani zipo taarifa za baadhi ya wabunge na wawakilishi kutoelewana katika majimbo yao jambo ambalo linahitaji kuepukwa kwani linaweza kukisababishia Chama cha CCM kufanya vibaya katika uchaguzi Mkuu ujao.
Alisema tahadhari lazima ichukuliwe kuhakikisha tofauti walizonazo zinaondoka na kukubali kufanyakazi kwa pamoja, kwani CCM ijayo itahakikisha haitawapa nafasi viongozi wababaishaji kwani imo katika kundaa mpango utakaotumika kupata viongozi katika kura ya maoni.
Hata hivyo Balozi Seif aliwatoa wasi wasi wabunge hao juu ya maendeleo ya matayarisho ya mswaada wa katiba mpya ambapo alisema kuwa tayari yapo katika hatua nzuri na ushiriki wa Zanzibar pamoja na maoni yao yameweza kuwasilishwa namna ya mchakato huo unavyotakiwa uende.
Alisema wanacho subiri hivi sasa ni kuona nini serikali itaamua baada ya mapendekezo hayo kufikishwa mbele ya serikali zote mbili na kuwataka wabunge hao kusubiria matokeo hayo.
Nae Naibu waziri wa Fedha katika Serikali ya Muungano, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Pereira Silima, akitoa shukrani zake alisema watahakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwa kuwatumikia vyema wananchi.
Alisema nia yao ya kuomba kuchaguliwa kuwatumikia wananchi ni kutokana na kuwa na nia ya kuwasaidia kuondokana na matatizo waliyonayo na watahakikisha kuwa wanashirikiana na kuona wanautumia vyema mfuko huo kuondoa matatizo yao
Labels
- .
- `
- 8
- AFYA
- AFYA.
- AJALI
- BIASHARA
- BURUDANI
- DINI
- ELIMU
- FILAMU
- HABARI
- HARUSI
- HOSPITALI
- I
- JAMII
- KATUNI
- Kii
- KILIMO
- KIMATAIFA
- KITAIFA
- Ku
- MAGAZETI
- Mahkamani
- MAISHA
- MAKALA
- MAKALA AFYA.
- MAKALA.
- MATUKIO
- MATUKIO.
- MICHEZO
- MITAANI
- MIUNDOMBINU
- MSAADA
- Ok
- SIASA
- TANGAZO
- TAWA YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI
- TEKNOLOJIA
- UCHUMI
- UTAFITI
- UTALII
- VIDEO
- VIJANA
- VISA INTERNATIONAL YAZINDUA TAWI TANZANIANa Mwandishi wetu 16.07.2025DAR ES SALAAM
- WEZI
Tafsiri ya Lugha
Popular Posts
- 
Mtaalamu wa lugha ya Alama Masika Khamis Ali akitoma maelezo kwa Wananchi wa makundi maalumu wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Kampeni wa Cha...
- 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uch...
- 
Na Mwandishi Wetu WMJJWM- Njombe Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Mkaundi Maaalum Dkt. John Jingu, amewataka...
- 
Dar es Salaam. 28-10-2025 Tanzania Bloggers Network (TBN) inatoa pongezi za dhati kwa Watanzania wote, wagombea, vyama vya siasa, Tume Huru ...
- 
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marce...
- 
Msanii wa Bongo Fleva Nandy akiburudisha kwa wimbo wake wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein A...
- 
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na hofu ya ulinzi na usalama wao siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025 na limewasihi wakapige kura n...
- 
Shamrashamra za ufungaji wa mkutano ya Kampeni wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) za Ubunge,Uwakilishi na Udiwani Jimbo la Chumbuni Zanzibar , kwa ...
- 
Shamra shamra wakati akiwasili Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BLOGU RAFIKI
- 
- 
Rais na Mgombea wa nafasi ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan apiga Kura katika Kituo cha Ofisi ya Kijiji Chamwino mkoani Dodoma - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) M...1 day ago
- 
Elimu : Bajeti za Elimu Zisipuuzwe wakati wa misukosuko ya Kiuchumi na Kisiasa Duniani - Kikwete na Malala Waonya. - Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai, wameonya juu ya mwenendo hatarishi duniani wa kupunguza au ku...1 week ago
- 
MAHOJIANO YA TAUSI SUEDI NA AMRI NGOYE KUHUSU CSI KUPITIA KWANZA PRODUCTION NCHINI MAREKANI - Pata habari motomoto kupitia facebook kwa kulike huu ukurasa wetu https://www.facebook.com/pages/Pamojapureblogspotcom/312633955485619?ref=hl7 years ago
Marafiki Duniani
Popular Posts
- 
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Zanzibar majira ya mchana kwa Ndege na kuendelea na taratibu za Maziko yatafanyika katika Mtaa wa...
- 
The United Republic Of Tanzania National Examination Council of Tanzania Form Four Examination Results 2017/2018 The National E...
- 
Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Zanzibar na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhani Haji Faki...
- 
Na Miza Kona/Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar Jumla ya wanafunzi 16,744 wamechaguliwa kuendelea masomo ya kidatu cha tatu kati ya wanafun...
- 
Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofa...
- 
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi
- 
Hutuba ya Mhe Waziri wa Afya Nd. Mahmoud Thabit Kombo kwa Waandishi wa Habari Katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Dunia Zanzibar, 22...
- 
Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za K...
 

 
.jpeg) 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment