Habari za Punde

MAZINGIRA KUINGIZWA MITAALA VYUO VYA UANDISHI HABARI

Na Mwantanga Ame

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) linakusudia kuingiza mtaala mpya katika mafuzo ya uandishi wa habari utakahusisha somo la mazingira.

Katibu wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga, alitoa changamoto hiyo wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa Habari waliokuwa wakipata mbinu mpya za Uandishi wa makala za kisayansi yaliofanyika katika Afisi za Baraza hilo Mwenge, Dar es Salaam.

Kajubi, alisema baraza limeamua kuingiza mtaala huo katika Vyuo vya Habari vya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwa ni hatua inayokusudia kuwapa waandishi wa habari mwanga wa kuandika taarifa za Mazingira.

Alisema baraza hilo linakusudia Watanzania wapatiwe taarifa zinazohusu mazingira kwa upeo mkubwa zaidi na hilo litawezekana zaidi endapo waandishi wa habari watakuwa wamebobea somo hilo.

Alisema kufikiwa kwa lengo baraza limefanya mawasiliano na Baraza la Mitihani la taifa Tanzania NECTA kuhakikisha mabadiliko hayo yanafanyiwa kazi.

Alisema wakati wowote mchakato wake utapokamilika Vyuo vyote vya mambo ya habari Bara na Zanzibar vitalazimika kuufuata utaratibu huo.

Mapema Mkufunzi katika Warsha hiyo, Mhadhiri wa Chuo cha Tumaini kanda ya Dar es Salaam Agnes Shija, akitoa maelezo yake juu ya habari za utafiti wa kisayansi alisema Waaandishi wengi wanashindwa kuandika habari za kisayansi kunakosababishwa na baadhi ya watafiti kuwa wagumu kushirikiana na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.