Habari za Punde

SABA WAJITOSA UCHAGUZI TAIFA JANG'OMBE

Na Mwajuma Juma

JUMLA ya wanamichezo saba wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa timu ya Taifa ya Jang'ombe unaoandaliwa kufanyika baadae.


Katibu wa muda wa timu hiyo Peter Augostino ameliambia gazeti hili kuwa kati ya wanamichezo hao, ni watano tu ndio waliobainisha nafasi watakazogombea, huku wawili wakiamua kufanya hivyo watakaporejesha fomu hizo.

Augostino alimtaja Yussuf Juma Mtumwa kuwa anakusudia kugombea kiti cha Katibu Mkuu huku yeye amechukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi.

Wengine waliochukua fomu na nafasi wanazoomba zikiwa kwenye mabano, ni Simon Benedicto, Mohammed Benedicto (Mwenyekiti), Haji Majid (Mjumbe), na Mohammed Juma Haji na Mohammed Chikambi ambao hawakutaja nafasi watakazowania.

"Hadi sasa wanachama saba wameshachukua fomu lakini wawili wameweka siri nafasi wanazozitaka hadi watakaporejesha fomu", alisema.

Uamuzi wa kufanya uchaguzi, umekuja kufuatia kauli ya Mbunge wa jimbo la Mpendae Salum Turky kwamba yuko tayari kuidhamini timu hiyo kwa sharti kuwa iwe na viongozi wanaotambulika.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mara baada ya sikukuu ya Eid el Fitr, kwa lengo la kuleta mabadiliko ili irudi katika hadhi na kuwa miongoni mwa zile zinazoheshimika kisoka.

1 comment:

  1. Ah, chama langu la mtaani,bado lipo hai? ila nadhani ule uwanja pale mivinjeni utakuwa wote ushajengwa nyumba toka miaka ile....lkn chama lile lina wapenzi,..du..we acha tuu!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.