Mheshimiwa Dr. Ali M. Shein;
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa BLM,
Ikulu,
Zanzibar.
Mheshimiwa Rais,
Viongozi na wanachama wa Zanzibar Welfare Association(ZAWA UK) tumezipokea habari za kuzama kwa meli ya Spice Islands kwa huzuni, masikitiko na unyonge sana.Aidha, tumepata maumivu sana kwa vifo vya wananchi wengi ambao walikuwa wakisafiri katika chombo hicho.
Haya ni maafa ni maafa makubwa kwa nchi yetu, Watanzania na Wazanzibari kwa ujumla wapo na ndugu zao kwenye katika kipindi hiki kigumu. Kwa niaba ya Jumuiya yetu ya ZAWA UK, nachukua fursa hii kutumia salamu za mkono wa pole na kwa kupitia kwako naomba utufikishie salamu za rambi rambi kwa ndugu zetu waliofiliwa na jamaa zao. Tunaomba wafahamu kuwa huu ni msiba wetu sote hata kama sisi tupo na nyumbani lakini machungu yake tumeyapata hadi huku tuliko.
Ama kwa ndugu zetu walionusurika tunawapa mkono wa pole kwa misukosuko mkubwa iliowafika, sisi ndugu zao tulioko UK tunaungana nao katika kumshukuru Allah kwa kuokoa maisha yao na pia tunamuomba Allah awafanyie wepesi wa kupona ili wapate kushiriki katika ujenzi wa taifa letu.
Inshallah Mwenyezi Mungu awape wafiwa wote subira, stahmala na uvumilivu kwa msiba huo na awalaze marehemu wote peponi(Amin).
Mheshimiwa, naomba kuwasilisha mbele yako.
Ahsante,
Hassan Mussa,
Mwenyekiti,
ZAWA(UK)
No comments:
Post a Comment