Habari za Punde

JUMUIYA ZA CCM KUTATHMINI MAFANIKIO, CHANGAMOTO

Na Mwandishi wetu

KONGAMANO la Jumuiya za Chama cha Mapinduzi (CCM), kutathmini mafanikio na changamoto la Utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho katika kipindi cha mwaka mmoja wa ushindi wake, linatarajiwa kufanyika leo hapa Zanzibar.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari, iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Salama Aboud Talib, imesema Kongamano hilo la siku moja, litafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, kuanzia saa 4:00 asubuhi.


Amesema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, ndiye atakayelifungua Kongamano hilo na litafungwa na Mjumbe wa Kamati Maalum ya NEC, Organaizesheni Machano Othman Said.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa UWT Zanzibar amesema Kongamano hilo litajumuisha wana Jumuiya wa UWT, UVCCM na WAZAZI, ngazi za Wilaya na mikoa yote ya Zanzibar.

Amesema mada mbili zitawasilishwa ikiwemo ‘mafanikio na changamoto za Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha mwaka mmoja wa ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu uliopita (2010) pamoja na Historia ya CCM tangu TANU na ASP’.

1 comment:

  1. Miongoni mwa mafanikio makubwa ya CCM kwa hivi karibuni, ni kuendelea kuongoza visiwa vya Unguja na Pemba Lkn. changamoto kubwa zaidi ni kua na wanachama wengi na viongozi wasio na imani na chama'wadandia basi' ambao wamejiingiza CCM kwa vile ndio njia pekee ya kufikia malengo yao. Changamoto nyengine ni ile ya kua na viongozi wengi wasiosoma..hivi ni kwamba Wasomi hawajitokezi au wananyimwa nafasi za uongozi chanani?..CCM bara ni tofauti!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.