Habari za Punde

UJENZI WA BARABARA TANO WAZINDULIWA PEMBA

Bakari Mussa na Nafisa Madai, Pemba

SERIKALI ya imedhamiria kwa dhati kuhakikisha inawapatia maisha bora wananchi kwa kuzitekeleza ahadi za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara.

Akizungumza na masheha, viongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na watendaji wa wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kisiwani Pemba, Mkuu wa wilaya ya Micheweni, Juma Abdalla Ali alisema serikali itahakikisha inatimiza ahadi za kimaendeleo ilizozitoa kwa wananchi wake.


Mkuu huyo alieleza hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Pemba katika ukumbi wa hoteli ya Misali Sunset Beach kwenye hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara tano za mkoa huo.

Alisema uzinduzi wa barabara hizo unathibitisha serikali ilivyokuwa tayari kutekeleza miradi hiyo ambayo ilitoa ahadi kwa wananchi kuwa itaitekeleza.

Alisema kuwa ujenzi huo wa barabara utakaojengwa kupitia mradi wa malengo ya Milenia (MCC), alisema barabara hizo zitakapokamilika zitasaidia kuwapunguzia wananchi wa Pemba usumbufu usafiri.

“Dalili za mvua ni mawingu kwa jinsi maandalizi ya maradi huu yalivyoanza serikali na wananchi wote wa visiwani hivi tunaimani kubwa kuwa mradi utatekelezwa kama ulivyopangwa na kukamilika mapema zaidi na katika kiwango kilichokubalika kwa mujibu wamakataba”, alisema mkuu huyo.

Alifahamisha kuwa ni mategemeo ya serikali na wananchi wa Mkoa huo kuwa utekelezaji wa mradi huo watatumia raslimali zilizipo Kisiwani Pemba na nguvu kazi zilizopo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ili wananchi waweze kufaidika na kuona kuwa mradi huo ni wao.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Rajab Uweje kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo alieleza kuwa wizara imefarajika sana kuona mashirikiano ya awali na wadau ambao barabara hizo zitapita umekuwa nafaraja kwa vile wanapoitwa wanaitikia wito.

Hata hivyo aliwataka viongozi wakuu wa Mkoa huo kuwaomba wananchi kuwa mashirikiano ya hali ya juu ili kuhakisha ujenzi huo unafanyika kwa ufanisi na kwamba ujenzi huo unatekelezwa kama ilivypopangwa.

Alizitaja barabara hizo ambazo zimo katika mradi huo ni pamoja na Kipangani –Kangagani 2.7 km, Chwale –Kojani 1.9km, Mzambarau Takao- Pandani-Finya 7.9 km, Mzambarauni Karim-Finya- Mapofu 8 km, Bahanasa-Daya 6.7 km, pamoja na Makongeni-Daya-Mtambwe 7.1 km ambazo jumla zitakuwa kilomita 35 km ambazo zitaajengwa kwa kiwango cha lami.


Barabara hizo zitajengwa na kamapuni ya H. Young kutoka nchini Kenya kwa usiamamizi wa kampuni ya LEA ya India ambapo ujenzi huo utachukuwa muda wa miezi 18 kuanzia na kugharimu jumla ya shilingi milioni 38.247.

Aidha zaidi ya shilingi bilioni 4 zimetumika kwa kulipwa fidia kwa wananchi ambapo Machi 2013 unategemewa kukabidhiwa mikononi mwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa upande wake mkandari wa ujenzi huo Michel Kitungu alisema kampuni yake itajitahidi kujenga barabara hizo kutokana na makubaliano ya mkataba waliowekeana na serikali na kuhakikisha kuwa hawataondoa njiani kwani kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa wa kazi kwa miaka 60 sasa.

Aidha alisema kampuni yake itatoa ajira ambazo hazitahitaji utaalamu kwa wenyeji wa maeneo husika kwa kutoangalia jinsia ambapo alisema kampuni yake itaangalia zaidi utendaji wa mtu mwenyewe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.