UJUMBE mzito wa viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar unatarajiwa kuondoka visiwani hapa kesho kuelekea Beijing, China kwa ziara ya mafunzo ya wiki mbili.
Wakiwa nchini China viongozi hao watajifunza mambo mbali mbali ya kiutendaji pamoja na kutembelea maeneo muhimu ya uwekezaji yanayotegemewa kwa uchumi wa China.
Viongozi hao pia watapata fursa ya kutembelea mji Shanghai na Suzhou ambapo watatembelea sehemu muhimu ikiwemo baadhi ya viwanda.
Miongoni mwa viongozi watakaokuwemo katika ziara hiyo ni pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, ambaye atakuwa ndiye mkuu wa msafara huo akisaidiwa na waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna.
Mbali ya waziri Shamuhuna msafara huo utakuwa na mawaziri wengine saba na naibu waziri mmoja wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wengine ni wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, maofisa na watendaji waandamizi katika wizara mbali mbali pamoja na waandishi wa habari.
Akizungumza kwenye mkutano maalum wa kuwaaga viongozi hao, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee alisema zaira hizo ni muhimu kwa viongozi hao.
Alisema kwa kiasi kikubwa China imepiga hatua za maendeleo ya kichumi na kijamii, hivyo Zanzibar nayo kama inataka kuendelea ni nafasi ya viongozi hao kujifunza na kuja kuitumia taaluma hiyo katika kuibadilisha Zanzibar.
“Tukayachukueni yale wenzetu wa China yaliyowawezesha kuendelea na tuyalete nyumbani kwa ajili ya kustawisha maisha ya nchi yetu”, alisema Omar Yussuf.
Ujumbe wa viongozi hao utarejea nchini Disemba 20 mwaka huu.
Mimi naamini hakuna cha kujifunza zaidi China, matatizo yaliyopo znz utatuzi wake unahitaji tu 'common sense' Hivi kwa mfano, kwa waziri wa Ardhi kuwaamuru watu wote wanaotaka kukata viwanja ktk mashamba yao wasifanye hivyo kabla ya kuishauri wizara husika ili kuepuka watu kuuza viwanja ktk maeneo ya kulima(mabonde) kweli inahitaji kwenda china? Ardhi yenyewe chache, ina jengwa ovyo ovyo..Hii imekua nchi ya bunuasi!..Tumemaliza bububu,mwera,fuoni sasa mwelekeo Jia la fumba!...viongozi kimyaaa!
ReplyDeleteNinakupongeza sana ndugu mwandishi kwa kuongea ukweli ulio wazi kabisa. Lakini zaidi ni kwamba hao viongozi wetu wanaokwenda huko China basi hawana kiu au niseme hamu ya kwenda kujifunza chochote huko kwa manufaa ya nchi. Safari hiyo ni kwa manufaa yao binafsi. Viongozi wachache sana katika serikali hii tuliyonayo wana uchungu na uzalendo na nchi hii. Hivi kuweka mji wetu katika mazingira mazuri na usafi inahitaji kujifunza China.
ReplyDelete