Habari za Punde

WAGENI WANAOJIFUNZA KISWAHILI TAKILUKI WAVUTIWA NA UFUNDISHAJI

Na Madina Issa

MKURUGENZI wa Taasisi ya kiswahili na lugha za Kigeni (TAKILUKI) Mmanga Mjengo Mjawiri amesema Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kitafanya mabadiliko katika sekta ya Elimu kupitia lugha ya kiswahili kwa wageni.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa akikabidhi vyeti kwa wanafunzi wa lugha hiyo kutoka katika chuo SOAS cha nchini Uingereza ambao walikuwepo Zanzibar kujifunza Kiswahili.
Alisema mabadiliko katika chuo hicho ni muhimu kwani itakifanya chuo kupelekea hata kukuza elimu katika vyuo tofauti nchini.

Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa wanatarajia kuanzisha diploma ya kiswahili kwa wenyeji na wageni ili waweze kupata wasomi wazuri na watafiti mbalimbali wa lugha hiyo.

Aidha Mjawiri amewataka walimu wa chuo hicho kutumia njia za kisasa wakati wanapowasomesha wanafunzi wa kigeni lugha ya kiswahili.

"Hivi sasa lazima walimu wa lugha wa chuo hichi watumie njia za kisasa wanapowafundisha kiswahili wageni kwani kitarahisisha ufahamu wao kuwa mkubwa katika kukijua kiswahili", alisema Mkurugenzi.huyo.

Hivyo ametoa wito kwa walimu wanaosomesha lugha kwa wageni wawe na utaratibu wa kujitathmini kwani itawasaidia hata kuwa na uzoefu mkubwa zaidi.

Akitoa shukurani kwa niaba ya wanafunzi wenziwe, Cathryn Bell amewapongeza walimu wa chuo hicho kwa utaalamu wao wa ufundishaji wa lugha hiyo kwani wameweza kujifunza lugha hiyo kwa ufahamu mkubwa.

Hata hivyo, aliahidi watakuwa mabalozi kwa wenzao ambao hawajapata mafunzo ya lugha hiyo kwa kuwasomesha na kuwafahamisha lugha hiyo.

Wanafunzi 9 kutoka chuo cha uingereza wamehitimu mafunzo ya kiswahili katika chuo hicho na kukabidhiwa vyeti vyao.

2 comments:

  1. Kiswahili sanifu na asili hakitafundishwa pahali popote katika dunia hii ispokuwa Zanzibar. Mola ibariki Zanzibar na watu wake Amiin.

    ReplyDelete
  2. Maneno yako ni kweli, lakini mwisho wa hilo unakaribia! Hatuwezi kuendelea kushikilia sifa ambayo, hatuifanyii kazi, wakati wenzetu wanajaribu kila wawezalo kukikuza na kukiendeleza Kisw. kwa kutumia vyombo vyao, ie. Vyuo vikuu, na vyombo vya khabari. SS. tumelala..fofofo. na hata vyombo vya khabari kwetu ni tatizo! Ukiomba kuanzisha chombo 'mbinde' Leo hii 'influence' ya KISW. cha bara imeenea kila kona. SS. tunalalamika tu..oh neno'kukarabati' si Kisw. lkn. wapi! Nakumbuka Siku moja Mw. wangu Mshindo alisema ktk. BBC, "wenye lugha hatuna vyombo, na wenye vyombo hawana lugha" Leo hii takriban tafiti zote za kisw. pamoja na vitabu vya kufundishia vyuo vikuu vimefanywa na watu wa nje ya Z'BAR. kama Dr. nchimbi na wengine, ukivisoma utumbo mtupu! kitaaluma wapo sawa lkn. hiyo ligha waliyoitumia kuieleza hiyo taaluma ndio utachoka. Hebu jamani serikali izinduke na kutumia 'comparative advantage' ijuilikane Z'bar ni Kiswa. na Kisw. ni Z'bar.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.