Habari za Punde

ZANZIBAR KUFAIDIKA NA UANACHAMA WA UMOJA WA NCHI ZA VISIWA VYA BAHARI YA HINDI

MSAADA WA BILIONI 12 ZANZIBAR-NA FAROUQ KARIM


NCHI TANO ZA VISIWA VILIOPO KATIKA BAHARI YA HINDI IKIWEMO ZANZIBAR VITAFAIDIKA NA MSAADA WA SHILLINGI BILLIONI 12 KUTOKA JUMUIA YA ULAYA  IKIWA NI KWA AJILI YA KUJIENDEELZA KATIKA MIRADI MINNE YA JAMII.


MSAADA HUO AMBAO UTAIPA FURSA ZANZIBAR KUFAIDIKA KATIKA SEKTA ZA MAENDEELO ENDELEVU.  MAAFA, MAZINGIRA NA MABADILIKLO YA HALI YA HEWA   UMETANGAZWA NA MRATIBU WA UMOJA WA NCHI TANO ZA VIISWA  UNAUJULIKANA KAMA SMALL ISLANDS DEVOLOPMENT STATES-SIDS-BW  SHAFICK OSMAN KUTOKA MAURITIUS WAKATI AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI KATIKA KONGAMANO MAALUM LA MRADI HUO.

BW OSMAN AMEWATAKA WANANCHI NA TAASISI ZA KIJAMII KUTUMIA FURSA HIYO KWA KUANGALIA  SEKTA AMBAZO ZINAHITAJI KUENDELEZWA  NA ZIWE ZENYE LENGO LA KULETA MABADILIKO NA KUONDOSHA UMASKINI HUKU AKISEMA TAASISI HIYO ITASHIRIKIANA NA SERIKALI  AMBAPO TAYARI  HATUA ZA AWALI ZIMEANZA

NAYE AFISA WA ELIMU NA MAZINGIRA AMBAYE NI MSIMAMIZI MKUU WA ZANZIABER BW HAMZA RIJALI AMESEMA ZANZIBAR IMEPATA  FURSA HIYO PEKEE KWA MARA YA KWANZA NA UZURI WA MRADI HUO  NI KUWA WANANACHI WENYEWE WATAYATAJA MAENEO AMBAYO YANATAKIWA KIUMARISHWA NA FEDHA HIZO ZITAGAWIWA KWA NCHI ZOTE KWA USAWA..


NCHI TANO ZA VISIWA  AMBAZO ZIMEUNGANISHWA KATIKA UMOJA HUO MBALI YA ZANZIBAR NI  MADAGASCAR, MAURITIUS, SEYCHELLES NA COMORO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.