Habari za Punde

Kuangamiza Misumeno ya Moto Hutumika Kinyume na Sheria za Utuzaji wa Mazingira ya Misitu.

 Baadhi ya Misumeno ya Moto iliyokamatwa na Maofisa wa Idara ya Misitu Zanzibar ikitumika kuangamiza misitu katika Visiwa vya Zanzibar, ambayo imepigwa marufuku matumizi yake bila ya kuwa na Kibali cha Matumizi ya msumeno huo.   
Wafanyakazi wa Idara ya Misitu wakiimwagia mafuta misumeno hiyo kwa ajili ya kuiangamiza, zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Misitu Maruhubi.
Kaimu Waziri wa Kilimo na Maliasili Ramadhani Abdalla Shabani, akiwa na mwenge wa moto tayari kwa kuiangamiza misumeno haramu a mbayo imekatazwa kutumika katika ukataji wa miti Zanzibar, kutokana na uharibifu wa mazingira ya misitu ya Zanzibar.zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Idara ya Misitu Maruhubi.

3 comments:

  1. Hii ndio akili ya mzanzibari jamani. Sasa kweni haiwezekani kuihifadhi hiyo misumeno, yanini kupiga moto? global warming ya bure? mnaharibu mazingira kwa piga moto kama hivi. eleweni!!!!!

    ReplyDelete
  2. mimi ni mzazibar halisa hapa jaamaa zangu mmechemsha yaani nimesikia uchungu inamaana viongozi akili hamna hii si ndio inachafua na kuzidi dhahma ya global warming akaaweeee naomba munitafutie namba ya hii oficeya kilimo

    ReplyDelete
  3. Ndio maana hatuendelei na hatutoendelea maisha! yaani hawa viongozi wazima wanathubutu kufanya haya ya kuchoma moto misumeno badala ya kuitaifisha ikaja kuifaa serekali kesho, Nchi yenyewe hata msumeno wa duni usio wa mashine mnaagizia Nje, leo mnaichoma hiyo kesho utaambiwa zimetumika Milioni kadhaa kuagiza vitendea kazi kutoka Nje...! Pumbavu..!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.