Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika majengo ya ZBC Rahaleo kutembelea Vyombo vya habari vilioko katika majengo hayo akiwa katika ziara ya Kikazi kutembelea Vyombo vya Habari vya Serikali Zanzibar.kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ali Mwinyikai.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea chumba cha habari cha Idara ya Habari Maelezo Rahaleo kuangalia utendaji wa kazi wa Idara hiyo.
Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti la Zanzibar Leo Abdalla Mohammed, akitowa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea chumba cha kutayarisha magazeti cha shirika hilo Rahaleo alipotembelea Ofisi hizi leo.
Mtayarisha Mkuu wa Chumba cha kutayarisha Gazeti la Zanzibar Leo Mohammed Othman, akitowa maelezo ya utayarishaji wa Gazeti la Zanzibar Leo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea chumba hicho akiwa katika ziara yake ya siku moja kutembelea vyombo vya habari Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maailm Seif Sharif Hamad, akielekeo katika jengo la Redio ZBC, Rahaleo baada ya kutembelea Ofisi za Zanzibar leo na Idara ya Habari Maelezo.
Mkuu wa Utangazaji ZBC redio Hassan Vuai, akitowa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea chumba cha kutangazia habari katika jengo la Redio Rahaleo.
Mhariri wa Habari wa ZBC redio Yunus Sose, akitowa maelezo ya utayarishajhi wa habari baada ya kukusanya na kupeleka kutangazwa redio, wakati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea kituo hicho.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar, akitowa maelezo ya jinsi Tume hiyo inavyofanya kazi kwa Wadau wake na usimamizi wa ugawaji wa mawimbi kwa vyombo vya habari Redio na TV,wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea tume hiyo Kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, Hassan Mitawi,akielezea utengaji wa kazi wa Shirika hilo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hame, alipotembelea kituo hicho Mnazimmoja akiwa katika ziara yake ya Kikazi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea chumba cha kurushia picha cha TV,akiwa katika ziara yake kutembelea vyombo vya habari vya Serikali Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wafanyakazi wa Chuo cha Habari Zanzibar baada ya kutembelea jengo hilo na kujionea jinsi ya utowaji wa Elimu ya Habari kwa Vijana wa Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar MaalimSeif Sharif Hamad, akiwa katika chumba cha kutangazia cha Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, akiwa na Mkuu wa Chuo hicho Saleh Mnemo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimsikiliza Fundi wa Kituo cha Redio Dole, akitowa maelezokuhusu utendaji kazi wa kituo hicho ambacho hutowa huduma ya kurusha matangazo kwa masafa marefu.kupitia mitambo hiyo mipya iliofimgwa hivi karibuni kutoka China.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam kutoka China na Mafundi wa ZBC, nje ya jengo la Redio Dole.
Fundi wa Kituo cha kurushia matangazo cha Masingini Ungja Khamis Ali, akitowa maelezo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais kituo hicho kinavyofanya kazi zake kutowa huduma za kurusha mawimbi ya picha za TV, na kuwafikia Wananchi.
No comments:
Post a Comment