Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, ajumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Hitma ya Mzee Karume Ofisi Kuu ya CCM Kisuwandui

Wananchi wa Mji wa Zanzibar wakiwa katika Viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui baada ya kughudhuria Hitma ya Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,iliofanyika katika jengo hilo.
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM,kughudhuria hitma ya Marehemu Baba yake Mzee Karume.Hufanyika kila mwaka 7Aprili ikiwa ni siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Mzee Karume.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ali Vuai , alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Kamanda wa JWTZ, alipowasili kudhughuria hitma ya Masisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu  Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM, Kisuwandui na kughudhuriwa na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Zanzibar.  
Mama Fatma Karume akisalimiana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali, alipowasili katika jengo la Afisi Kuu ya CCM kwa ajili ya kusoma hitma ya Marehemu Mzee Karume.  
Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM, kughudhuria Hitma ya Marehemu Mzee Karume, hufanyika kila mwaka 7,Aprili. ikiwa ni Kumbukumbu ya kumkumbuka Mzee Karume Mwanamapinduzi wa Zanzibar na Muasisi wa Maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pembe.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Chama na Serekali alipowasili katika Viwanja vya Jengo la Afisi Kuu ya CCM, kwa ajili ya kusoma hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.  
Rais Mstaafu wa Tanzania Alhajj Ali Hassana Mwinyi, akitia ubani kupiga Fatha katika kisoma cha Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, anaefuta Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuka na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama katika Hitma ya Marehemu Mzee Karume iliofanyika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM.

Mashekhe mbalimbali kutoka Zanzibar na Dar-es- Salaam, wakisoma hitma ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Wananchi wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisuwandui, wakisoma hitma ya kumbukumbu ya Mzee Karume. 
Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi  zao Zanzibar wakijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika kisomo cha hitma kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwa na Mawaziri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar katika kisomo cha hitma.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis, akisoma dua ya kuhitimisha hitma ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume










Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka shada la maua katika kaburi.
Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akiweka shada la maua kwa niaba ya Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi Mdogo wa Msumbiji Zanzibar  ambaye ni Kiongozi wa Mabalozi waliopo Zanzibar akiweka maua kwa niaba ya Mabalozi wenzake waliopo Zanzibar.
Mtoto wa Marehemu Mzee Karume Balozi Ali Karume akiweka shada la mau katika kaburi la Baba yake baada ya kumalizika kwa hitma iliosomwa katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. 
Mjukuu wa Marehemu Mzee Karume Ahmed Amani Karume , akiweka shada la mau kwa niaba ya Wajukuu wote.
Viongozi wakiitika dua wakiwa katika kaburi, kutoka kulia Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Balozi Mdigo wa Msumbiji Benard Costantino na Mtoto wa Mzee Karume Balozi Ali Karume. 
Shekh. Al-Haady Mussa wa Mkoa wa Dar-es- Salaam,akisoma dua katika kaburi la marehemu Mzee Karume baada ya kumalizika kisomo cha hitma.
Wananchi na Waheshimiwa wakiitikia dua katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisuwandui.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Omar Kabbi, akisoma dua katika  kaburi la Marehemu Mzee Karume. 
Mchngaji wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Zanzibar Fr. John Shayo akimuombe Mzee Karume. kwa madhehebu ya dini yake.    
Mama Fatma Karume akijumuika na Wake wa Viongozi na Wananchi waliofika katika kisomo cha hitma kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM.
Mtoto wa Mzee Karume Balozi Ali Karume, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika kisomo cha hitma Afisi Kuu ya CCM,  na kuelezea wasifu wa Mzee wake wakati wa uhai wake.  
Rais Msataaf wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, akizungumza na mwandishi wa chanal ten Munir Zakari, baada ya kumalizika kwa dua ya kumuombea Mzee Karume iliofanyika katika Jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.  
Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Mwinyi Sadala, akifanya mahojiano na Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni, katika viwanja vya CCM, ambaye ni Mwakilishi wa Kuteuliwa kuipitia Chama cha CUF.
Mabalozi na Wananchi wakiwa katika Viwanja vya Afisi Kuu ya CCM, wakibadilishana mawazo baada ya kulalizika kwa kisomo cha hitma na dua. 
Wanafunzi wa Madrasa mbalimbali za Zanzibar walishiriki mkatika kisomo hicho.wakiwa nje ya jengo baada ya kumalizika kwa kisomo hicho.

1 comment:

  1. Chonde chonde ndugu zangu Waislamu. Tungelikuwa tunaiga mambo mengi mazuri tungelikuwa mbali.

    Ya kuyatanabahisha ni kuwepo kwa Sanamu la Karume (Sijui linamsaidia vipi marehemu maana Sala ya Idd ilibidi kuhamishwa Afisi Kuu kwa sababu ya kuwepo sanamu hili na bado lipo na Masheikh wanahudhuria) . Kuweka mashada ya maua (si mila zetu hizi Waislamu) Kuienzi kila siku ya tarehe 07/04 ( hatuna mambo haya katika uislamu) Kusoma khitma kila mwaka( Ni Karume pekee anaefanyiwa hili na halina mashiko).

    Serikali si ya kiislamu ila wanaserikali ni Waislamu na wana masuuliyah, wanatanabahi?

    Hatuwezi kupata utaratibu mwengine wa kumuenzi Muasisi wetu ambao hautokuwa unapingana na taratibu zetu za kidini?

    Kwanini hatuyaigi yale yanayoendana na misingi yetu ya kidini na Hadithi ya Mtume wetu rahma na amani juu yake imesema anapokufa binadamu amali zake zote hukatika isipokuwa kwa mambo matatu...

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.